Header Ads Widget

WANANCHI VISIWANI ZANZIBAR WAMETAKIWA KUDUMISHA AMANI ILI KUIMARISHA MSINGI WA MANDELEO YA TAIFA


Matukio Daima App, Zanzibar.

WANANCHI Visiwani Zanzibar wametakiwa kudumisha Amani na Mshikamano uliopo ili kuimaeisha Msingi wa Maedeleo ya Taifa.


Wito huo umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza wakati wa ziara maalum ya kuwatembelea Wazee, Wagonjwa na Watu wasiojiweka katika Jimbo hilo ambapo amesisitiza Umoja na Mshikamano ili taifa lisonge mbele.


Amesema,  Mafanikio Katika taifa yanapatikana endapo Wananchi kuanzia ngazi ya Chini wanakuwa wamoja na wenye kudumisha Amani.


"Mimi nataka kusema kwamba, Mafanikio yoyote yanapatikana endapo tutashirikiana kwa umoja wetu na upendo ambao hata Marais wetu wote wanasisitiza jambo hilo," amesema.


Amefafanua kuwa lengo la kufanya ziara ya kuwatembelea wazee, Wagonjwa na kaya Masikini ni muendelezo wa kuwaunganisha Wananchi wa Jimbo la Chumuni pamoja.

"Huu ni muendelezo wangu kwa Wananchi wa Jimbo la Chumbuni ambapo kwa pamoja tutafurahi pamoja kwa kusaidiana chochote tulichokuwa nacho," ameeleza.


Kwa upande wao Wazee, Wagonjwa na Watu wasiojiweza katika Jimbo la Chumbuni wamemmshukuru Mbunge huyo kwa hatua aliochukuwa ya kuwatembelea pamoja na kuwapatia msaada wa vitu mbalimbali.


"Hatuna cha Kumlipa Mbunge wetu, kikubwa tunamuombea Umri mrefu kwa Mwenyezimungu kwa msaada wa vyakula aliotupatia.


Katika Ziara hiyo Mbunge huyo alitoa Msaada wa Vyakula, Sabuni na Fedha taslim kwa makundi mbalimbali ya Watu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI