Na Gift Mongi,MATUKIODAIMA APP MOSHI.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Kilimanjaro Shally Raymond amewahakikishia wananchi wa kata ya Uru Kusini kuwa ataendelea kusaidiana na mbunge kuhakikisha maendeleo yanakuja kwa kasi Moshi Vijijini.
Mbunge anatoa kauli hiyo mbele ya wananchi wakijitokeza katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi uliofanyika katika kijiji cha Kitandu.
'Niseme tu nimefurahishwa na Kasi ya maendeleo iliyopo na mimi kama mbunge nitaungana na mwenzangu ili kuleta maendeleo kwa kasi zaidi'alisema
Kwa upande wake katibu wa chama cha mapinduzi (CCM)wilaya ya Moshi Vijijini Ramadan Mahanyu mbali na kuwapongeza wabunge hao kwa uchapaji kazi wao katika kuleta maendeleo pia aliwataka wananchi kuwaunga mkono.
'Mnatakiwa kuwaunga mkono sasa kwa namna wanavyojitoa na kuhakikisha maendeleo yanapatikana ili kuweza kuwatia moyo'alisema
Diwani wa kata ya Uru Kusini Wilhad Kitaly alimshukuru mbunge Prof Patrick Ndakidemi kwa kufanya ziara kwenye kata hiyo jambo linalotia motisha zaidi kwenye maendeleo.
"Tunashukuru kwa ambavyo ungekuwa mstari wa mbele kututoa moyo katika nyanja ya kimaendeleo tukuhakikishie tu sisi wana Uru Kusini hatutakuangusha hata kidogo 'Anasema
Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick ameonyeshwa kuridhishwa kwake Kwa namna wananchi wanavyojitoa katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo
'Lazima tuishukuru serikali ya rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ambavyo imekuwa na hicho la pekee katika kata yetu na jimbo kwa ujumla katika kutuletea fedha za miradi mbalimbali'alisema
Hata hivyo mbunge huyo aligawa miche ya kisasa ya migomba kwa viongozi wa kata hiyo kwa lengo la kuhamasisha kilimo cha kisasa ambacho kinaweza kumuinua mkulima.
Mwisho.
0 Comments