Na Mwandishi wetu, Lindi
Juisi iliyotengenezwa kwakutumia viazi lishe vilivyofanywa utafiti kutoka TARI Niendelee imekuwa kivutio kwa watu wengi kutokana na radha pamoja na rangi huku wengi wakiona jambo geni kwa Viazi kutengenezea juice.
Akizungumza katika maonyesho ya wakulima katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi Mtafiti wa Zao la Viazi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania Tari kituo cha Naliendele Festo Masisila alisema kuwa juisi hiyo ni mkombozi wa watu wenye matatizo mbalimbali kiafya wakiwemo watoto wadogo wasioweza kutafuna ambapo Ina virutubisho vingi Bora kwa Afya.
"Sisi tumejikita kwenye mihogo na viazi vitamu tuna mbgu bora za viazi zaidi ya 10 ambao zipo zenye viinilishe vya vitamin a wengi huita viazi lishe hizi mbegu bora zilizodhibitishwa na tosci ni pamoja na tari sp 1-7, taya”
“Zipo zenye viinilishe vingi na zinasaidia watoto wajawazito na wazee au wale wenye magonjwa hasa yanayosababihjsa kushuka kwa kinga za mwili na uono hafifu”
"Tumekuja na juice ili kuisindika an kuifanya juice iweze kutumiwa na kila mtu lakini kiazi kitamu kina wanga kwa asilimia kubwa ambapo huongeza virutubisho mara dufu mwilini”
“Namna gani unaweza kuzalisha ambapo uzalisjaji wake ni mkubwa ambapo huzalishaj zaidi ya tani 8 -13kwa mbegu za kisasa ambazo hukomaa ndani ya miezi 4 tani 3-4 hekta moja ukomaaji wake ni wamuda mfupi ambao mkulima hupata pesa”
"Serikali imekuwa ikitoa pesa kwaajili ya kutumia chanjo ya matone ya vitamin A tukiongeza hamasa ya kulima zao la viazi tunaweza kufanya vizuri zaidi na kuipunguzia gharama serikali kwa kiwango kikubwa ya kuagiza chanjo ya vitamin A" alisema Masisila






0 Comments