Header Ads Widget

FIGO YA NGURUWE KUTUMIKA KWA BINADAMU .



Na Simon Joshua - Matukio Daima App, Iringa.

Timu ya madaktari wa Marekani inasema figo ya nguruwe iliyokarabatiwa jeni na kupandikizwa kwa mtu mwenye ubongo uliokufa, imeendelea kufanya kazi kama kawaida kwa zaidi ya mwezi mmoja.


Timu hiyo inayoongozwa na madaktari wa upasuaji katika Chuo Kikuu cha New York nchini Marekani ilitoa matokeo hayo juzi Jumatano.


Figo ya nguruwe ambayo ilipandikizwa katika mwili wa Binadamu kwa zaidi ya mwezi mmoja, imefanya kazi kwa ufanisi ikiwa ni hatua ambayo Madaktari wa upasuaji wana matumaini makubwa kwamba siku moja wataweza kutumia aina hii ya upasuaji kuokoa maisha ya Binadamu ambao ni Wagonjwa.


Upasuaji huo wa majaribio ulifanyika kwa idhini ya Familia ya Mtu ambaye alikuwa ametangazwa kuwa ubongo wake hautaweza kufanya kazi tena na kuamua kutoa mwili wake kwa ajili ya tafiti za kisayansi.

Hospitali ya Chuo cha ‘NYU Langone Health’ cha Jijini Newyork nchini Marekani mapema wiki hii kimetangaza kuwa jaribio hili linaashiria muda mrefu zaidi wa figo ya nguruwe iliyotengenezwa kwa vinasaba kufanya kazi ndani ya mwili wa Binadamu.


Mwaka jana, Madaktari wa upasuaji wa Chuo Kikuu cha Maryland waliweka historia kwa kupandikiza moyo wa nguruwe ndani ya Binadamu aliyekuwa anakaribia kupoteza maisha yake ambapo aliweza kuishi kwa muda wa miezi miwili kabla ya moyo huo kuacha kufanya kazi kwasababu ambazo hazieleweki kikamilifu mpaka sasa lakini hatua hiyo inatumika kwa ajili ya mafunzo ya majaribio yajayo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI