Header Ads Widget

CHANGAMOTO YA MAJI KUTATULIWA MOSHI.

 


Na Gift Mongi-Matukio Daima App, Moshi.


Kutokana na uhaba wa maji unaozikumba kata za Kibosho Okaoni, Kibosho Kati na Kibosho Kirima zilizopo tarafa ya Kibosho, Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi amesema siku chache zijazo RUWASA wataanza kutekeleza ujenzi wa mradi unaokwenda kutatua changamoto ya uhaba wa maji katika  Kata za Kibosho Okaoni, Kibosho Kati na Kibosho Kirima.


Kauli hii ya matumaini inathibitishwa na meneja wa Ruwasa Wilaya ya Moshi mhandisi. Musa Msangi ambaye alikuwa kwenye hafla ya kupokea vifaa vya mradi utakaopeleka maji katika  kata za Kibosho Okaoni, Kibosho Kati na Kibosho Kirima.


Hafla hiyo ilifanyika katika uwanja wa Makondoo katika Kata ya Kibosho Kirima ambapo mhandisi Msangi aliishukuru Wizara kwa ushirikiano mkubwa aliopata katika kutekeleza mradi huo.


Kadhalika  Aaliwaomba viongozi wote wa Kata na Vijiji kumpa ushirikiano anapowajengea mradi huo ili kuweza kuleta tija kama ilivyokusudiwa


Akizungumza  baada ya kupokea vifaa vya kujenga mradi  huo, Prof Ndakidemi amemshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kiasi cha shilingi milioni 438 kutekeleza mradi wa kutatua changamoto ya maji katika Kata za Kibosho Okaoni, Kibosho Kati na Kibosho Kirima.


“Kipekee kabisa nimefarijika sana kupokea vifaa vya mradi huu kutoka Serikalini. "Amesema Mhe. Ndakidemi".


Akizungumza mbele ya viongozi wa Vijiji vya Otaruni, Maua, Uchau, Kirima na Boro na wale  wa Jumuiya ya watumia maji ya SIKIKA, na Mtendaji wa Kata na wale wa vijiji, Prof  Ndakidemi amewaomba viongozi hawa wakaelimishe wananchi kuhusu umuhimu wa mradi huu unaokwenda kutatua changamoto ya maji katika maeneo yao.


Amewaomba wananchi wote wakawe walinzi wa miundombinu ya  huo mradi ili kuwa endelevu Kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Kwa nyakati tofauti, Madiwani wa Kata za Kibosho Kirima na Kibosho Kati waheshimiwa Inyasi Stoki na Bahati Mamboma walimshukuru Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia pesa za kutekeleza mradi huo. Vilevile walimshukuru mbunge kwa kufuatilia fedha za mradi huo.


Kwa namnavya pekee kl walimshukuru mhandisi Musa MsangiI kwa jinsi anavyowapa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao.


Wenyeviti wa Vijiji vya Maua, Otaruni, Uchau Kaskazini, Uchau Kusini, Kirima Juu, Kirima Kati na Boro nao walimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha za kuwajengea mradi wa maji. Waliahidi kuwa watakuwa walinzi wa huo mradi na watashirikiana na serikali katika hatua zote za utekelezaji.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI