Header Ads Widget

AMUUA MKE WAKE NA SHEMEJI YAKE KWA AJILI YA IMANI YA KISHIRIKINA.

 


Na Amina Saidi,Matukio Daima App,Tanga

Jeshi la Polisimkoa wa Tanga limefanikiwa kumkamata Swalehe Miraji Ally mwenye umri w miaka (38)kwa kosa la kumuua mke wake pamoja na shemeji yake  kwa kuwakata panga kichwani mara mbili wakati wakiwa shambani na kukimbilia mkoani Tabora


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya taarifa hiyo kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Tanga ACP Alma Almachius Mchunguzi amesema kuwa mtuhumiwa ambaye ni fundi ujenzi mkazi wa Mkanyageni Wilayani Muheza alimuua mkewe Mwanahawa Hassan(24)kwa imani za kishirikina na shemeji yake Sauda Sufian (20)kisha kukimbilia Tabora lakini jitihada za Polisi zilifanikiwa na kumkamata mtuhumiwa huyo  kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria


Pia katika taarifa nyingine kamandq Mchunguzi amesema kuwa jeshi hilo limefanikiwa kuwatia hatiani watu watano kwa makosa mbali mbali ambapo Ally Kilulu amehukumiwa miaka 15 jela kwa kosa la kupatikana na dawa za kulevya aina ya Heroin gram 1,Amos Hamis akihukumiwa miaka 14 jela kwa kosa la kubaka huku Halidi Yusufu akihukumiwa miaka 5jela kwa kosa la wizi wa mifugo


Aidha Jeshi hilo wilayani Handeni limefanikiwa kumkamata Rajabu athuman mwenye umri wa miaka 32 kwa kosa la kumuua kwa kumkata kichwa Helen Sila ambapo bado upelelezi unaendelea kufuatia tukio hilo


Sambamaba na hayo Kamanda Mchunguzi amewataka wananchi mkoa wa Tanga kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama pale wanapona  viashiria vya uharifu wa amani katika maeneo yao ili sheria kali dhidi ya wahalifu ziweze kuchukuliwa


Jeshi linatoa  wito kwa wananchi wote mkoani Tanga kuendelea kutoa ushirikiano wa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa Jeshi la polisi ili kuzifanyia kazi na kuimarisha hali ya utulivu na amani


"Wananchi wote mkoa wa Tanga muendelee kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi katika maeneo yenu na kuwatumia wakaguzi kata wa Jeshi la Polisi waliopo katika kata zote mkoani hapa katika kuzuia viashiria vya uhalifu kabla haujatendeka katika maeneo yenu"alisema Mchunguzi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI