Na Fatma Ally, Matukio DaimaApp, Dar
CHAMA cha Act Wazalendo kimeishauri Serikali kuchukua hatua za haraka ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa mafuta ya disel na petrol ambapo mafuta yaliopo nchini yanaweza kukidhi kwa siku 8 tu na sio mwezi mmoja kama ilivyozoeleka.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Waziri kivuli wa sekta ya Nishati Isihaka Rashid Mchinjita amesema kuwa sababu kubwa inayopelekea tishio la ukosefu wa mafuta ni kupungua kwa uwezo wa wa kuagiza mafuta kwa waagizaji wa ndani.
Amesema kuwa, katika utafiti uliofanyw na Chama hicho umebaini kuwepo kwa uhaba wa mafuta ya disel na petrol ambapo katika bandari ya mtwara hali imekua mbaya zaidi, hivyo hupelekea kwenda bandari ya Dar es Salaam.
"Tangu mwezi Machi kutokana na uhaba wa dola waagizaji wamekua wakipunguza kiasi wanachoagiza, hii ni kutokana na uhaba wa dola za Marekani na kushuka kwa thamani ya shillingi ya Tanzania " amesema Waziri kivuli Mchinjita.
Aidha, amesema ni wakati wa Serikali kueka msisitizo wa kupunguza matumizi ya mafuta ya petrol na disel kwenye magari yote ya Serikali kwa kutumia nishati mbadala ya gesi asili, ambapo bohari zote za serikali (GPSA) zifungwe mitambo ya kujazia gesi asilia.
Ameongeza kuwa, tatizo la upatikanaji wa mafuta na gharama zake linahitaji hatua za makusudi za serikali, licha ya kuwa tatizo la uhaba wa dola linazikumba nchi nyingi lakini Tanzania haipaswi kukaa kimya licha ya kuchukua hatua za kisera na kikodi.
"Changamoto ya upatikanaji wa mafuta imepelekea waagizaji hususani wadogo kuchelewa kupata mzigo kutoka bohari za Dar es Salaam ambapo awali ilikua inachukua siku moja tu lakini ni siku 3 hadi 4"amesema Waziri kivuli Mchinjita.
Hata hivyo, amesema ni vyema Serikali ikaweka vivutio katika sekta ya utalii na ikaongeza matangazo na kuboresha miundombinu ya utalii lengo ikiwa ni kuongeza idadi ya watalii waliopo sasa






0 Comments