Na Simon Joshua-Matukio Daima App, Ukraine.
Idara ya usalama ya Ukraine imesema mwanamke mmoja amekamatwa kwa madai ya kushirikiana na Urusi na kula njama ya kutaka kumuua rais Volodymyr Zelensky.
Idara hiyo imesema, mwanamke huyo kabla alijaribu kujua ratiba ya Rais Zelensky huko Mykolaiv ambayo ilikumbwa na mafuriko mwezi Juni.
Ukraine mara kwa mara inashutumu wakaazi ‘wasaliti’ wa eneo hilo wanaounga mkono Urusi na kulisaidia jeshi la Moscow kwa kulipa taarifa.
Bw Zelensky alithibitisha kuwa alikuwa amefahamishwa kuhusu kukamatwa kwa mwanamke huyo akisema mkuu wa SBU alikuwa amemjulisha kuhusu "vita dhidi ya wasaliti".
Idara ya usalama ya Ukraine, SBU, ilisema katika taarifa yake kwamba mwanamke huyo alikamatwa baada ya kufumwa alipokuwa akijaribu kuwasilisha taarifa za kijasusi kwa Warusi.
Walidai kuwa kabla ya ziara hiyo, alijaribu kukusanya taarifa za kijasusi ili kujaribu kujua mipango ya Bw Zelensky katika eneo la kusini la Mykolaiv.
Pia walichapisha picha ya mshukiwa akiwa na maofisa wa SBU waliojifunika nyuso zao jikoni, wakificha pia tia uso wa mwanamke huyo na maafisa hao.
Bw Zelensky alitembelea Mykolaiv mnamo Juni kuona uharibifu uliosababishwa na bwawa la Kakhovka kumwaga maji baada ya kushambuliwa na Urusi na akatembelea tena Julai baada ya makombora makubwa ya Urusi.
Idara ya usalama ilisema ilifahamishwa kuhusu njama hiyo kabla ya ziara hiyo na kuongeza hatua za ziada za usalama.
Ilidai kuwa Urusi ilikuwa ikipanga "shambulio kubwa la anga kwenye eneo la Mykolaiv" na mshukiwa alikuwa akijaribu kuwapa taarifa kuhusu maeneo ya mifumo ya kivita ya kielektroniki na maghala yenye risasi ambazo zinaweza kulengwa na jeshi la Urusi.
Kulingana na SBU, mshukiwa huyo anaishi katika mji mdogo uitwao Ochakiv, ambao Bw Zelensky alitembelea mnamo Julai, na alikuwa akifanya kazi katika duka moja lililoko katika kambi ya kijeshi huko.
Inafahamika kuwa SBU haikumkamata mshukiwa wakati wa ziara hiyo na ilichukua hatua za usalama kuzuia shambulio dhidi ya rais wa Ukraine.
Maafisa walimfuata baada ya ziara hiyo ili kujua zaidi kuhusu matendo yake na "kazi zilizopokelewa" na Warusi, SBU iliongeza.
Taarifa hiyo ilidai kuwa mshukiwa aliendesha gari katika eneo hilo na alikuwa amepiga picha mnano na video za vituo vya kijeshi vya Ukraine.
Anatarajiwa kukabiliwa na mashtaka ya kusambaza habari kuhusu mienendo ya silaha na wanajeshi.
Iwapo atapatikana na hatia, anaweza kutumikia kifungo cha hadi miaka 12 jela.
Vikosi vya usalama vya Ukraine vimewakamata watu kadhaa wanaodaiwa kuwa ni "mawakala wa Urusi" ambao inaamini walikuwa wakitoa taarifa kuisaidia Urusi kufanya mashambulizi ya anga kulenga kambi na vituo vya silaha
0 Comments