Header Ads Widget

PROF NDAKIDEMI AKAGUA MAENDELEO CHUO CHA UFUNDI STADI KIBOSHO

 

Na Gift Mongi MATUKIO DAIMA APP MOSHI

Ni muendelezo wa  ziara ya mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali jimboni mwake lengo likiwa ni kujionea uhalisia wa miradi husika badala ya kusubiria kupelekewa taarifa pekee.


Mapema hii leo agusti 8.2023 mbunge huyo alipata wasaa wa kutembelea lakini pia kukagua 

 maendeleo ya Cchuo Cha Kibosho Vocational Training Center  kilichoko katika Tarafa ya Kibosho, Halmashauri ya Moshi vijijini Mkoani Kilimanjaro.



Aidha  Prof. Ndakidemi alitembea na kujionea miradi ya kilimo na ufugaji inayotekelezwa hapo chuoni na kuridhishwa namna wataalamu wa kilimo wanavyoandaliwa Kwa vitendo. 


'Binafsi mimi ni mbobezi katika sekta hii muhimu ya kilimo nimeridhishwa namna vijana wetu wanavyoandaliwa kivitendo na sii kinadharia pekee hakika tunaenda kuzalisha wataalamu wa kutosha katika sekta hii tegemezi'anasema Prof Ndakidemi


Ziara hii imekuaja kufuatia   waliko wa kukitembelea Chuo hicho kutoka kwa mkuu wa Chuo  Daniel Mboya ambaye alitamani kuona mwakilishi huyo kujua kile kinachozalishwa ama kufundishwa kwa wanafunzi chuoni hapo.


Aidha  kiwa hapo chuoni, mbunge alipata fursa ya kuongea na bodi ya chuo chini ya uenyekiti wa   Thomas Kimboka ambapo  katika kikao hicho,  alielezwa kuwa chuo kinakabiliwa na uhaba wa fedha za kakamilisha ujenzi wa baadhi ya miundombinu hapo chuoni.


'Naomba kuwapa ushauri mzuri tu kuwa   kuwa uongozi muitishe harambee na kuwakaribisha wadau mbalimbali ili tuchangishe fedha za kukamilisha huu ujenzi mara moja'anasema


Chuo cha  Kibosho Vocational Training Center kinamilikiwa na wananchi wa tarafa ya Kibosho yenye kata sita.


Mbunge huyo ameigawa   miche ya kisasa ya migomba kwa chuo na kwa wajumbe wa bodi lengo likiwa ni kuhamasisha kilimo cha kisasa cha zao la ndizi.


Mkazi wa Kibosho Ombeni Mushi amesema inaleta faraja kuona wawakilishi waliowachagua wanapoenda kuwatembelea na kusikilizwa kero zao tofauti na ilivyozoeleka kufuatwa ofisini.


'Tuseme tuna faraja kubwa Kwa kuwa na kiongozi anayetujali na anashuka hadi  ngazi za chini kutusikiliza huu ndio aina na uongozi unaofaa'anasema


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI