Header Ads Widget

WAKULIMA, WAFUGAJI NA WAVUVI WATAKIWA KUHIMILI MABADILIKO YA TABIANCHI


Na Hamida Ramadhan-Matukio Daima APP, Dodoma.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema kuwa Maonesho ya mwaka huu ya Kilimo Mifumo na Uvuvi yameandaliwa huku lengo likiwa ni kutoa ujumbe utakaowawezesha wakulima, wafugaji na wavuvi kuhimili mabadiliko ya Tabianchi.


Hayo ameyasema Leo Jijini hapa Wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu sherehe na maonesho ya nanenane Kanda ya Kati yatakayoanza Agosti 1 Hadi 8 katika viwanja vya nanenane Nzuguni.


Mkuu huyo amesema Mikoa ya Dodoma na Singida imeendelea kuathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kuathiri uzalishaji wa mazao ya kilimo mifugo na uvuvi.


"Mbinu hizo ni pamoja mbinu za hifadhi ya maji na udogo mashambani zikijumuisha matumizi ya makingamaji, kilimo cha mbegu tisa na jembe la mzambia, kuzalisha mazao yanayotumia maji kwa ufanisi (Mtama na alizeti), uzalishaji wa malisho kwa ajili ya mifugo, hifadhi ya misitu na upandaji wa miti, matumizi ya nishati mbadala (Jua, umeme na gesi) kwa ajili ya kupikia".


Amesema katika maonesho hayo wadau wataonesha teknolojia na fursa mbalimbali zilizopo katika mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi.


Ameeleza kuwa Maonesho ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Kanda ya Kati yanahusisha mikoa ya Dodoma na Singida mikoa yenye dhamana ya kuhakikisha Sherehe hizo za wakulima na wafugaji zinafanyika kwa ufanisi.


Kadhalika amesema katika maonesho ya mwaka huu tumejipanga kufanya yafuatayo Kuongeza hamasa ya uzalishaji wenye tija; Kutakuwa na Teknolojia mbalimbali za kuongeza tija na faida katika mnyororo wa thamani.


Wadau watapata fursa za kubaini teknolojia zitakazoongeza tija katika uzalishaji wao.  Kusambaza mbinu za kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi na uharibifu wa mazingira:


Aidha amesema ,katika maonesho hayo wadau hushindanishwa na kupata washindi kulingana na makundi ya bidhaa na teknolojia wanazoonesha.


"Washindi hawa hupata zawadi kulingana na uwezo wa kila Kanda na zawadi ambazo zimekuwa zikitolewa ni pamoja na Hati, Vikombe, na Fedha taslimu," Amesema Senyamule


AJIRA KWA VIJANA


Maonesho hayo yatatumika kuhamasisha vijana kujishughulisha na shughuli za kilimo, mifugo na uvuvi.


Amesema Halmashauri zitahamasisha vijana waliofanikiwa kuja kwenye maonesho kutoa ushuhuda wa namna shughuli zao zilivyowanufaisha. BBT ni mfano mmoja wa kuhusisha vijana katika kilimo.


Amesema usambaza teknolojia za kisasa katika kilimo na ufugaji bora;Katika maonyesho ya mwaka huu Makampuni na watu binafsi wameleta teknolojia bora za ufugaji wa mifugo, mbegu bora za mazao mbalimbali kwa kuzingatia vipaumbele vya mkoa wa Dodoma na Singida.


Amesema Taasisi za utafiti za kilimo, mifugo na uvuvi zinashiriki maonesho hayo kuonesha teknolojia mbalimbali zilizozalishwa kwenye vituo vya utafiti na kuwawezesha wakulima kunufaika na elimu ya uzalishaji bora.     


Amesema Matukio Muhimu kwenye Maonesho ya 2023Tofauti na Maonesho ya miaka iliyopita, maonesho ya Nanenane 2023 yatahusisha matukio muhimu na makongamano yanayoongeza wigo wa uzalishaji bora.


"Kongamano la Tasnia ya Alizeti Mikoa ya Dodoma na Singida ilikabidhiwa jukumu la kuzalisha alizeti kwa wingi ili kupunguza nakisi ya mafuta ya kula nchini na hivyo kuokoa fedha za kigeni zinazotumika katika uagizaji wa mafuta ya kula nje ya nchi," amesema Senyamule.


Na kuongeza "Mikoa hii iliandaa mikakati ya utekelezaji na hali inaonyesha kuongezeka kwa upatikanaji wa mafuta ya kula na bei kushuka kutoka shilingi 7,000 kwa lita na sasa ni wastani wa shilingi 4,000 kwa lita,"


"Siku  hii yatafanyika Maonesho maalumu ya zao la alizeti na kutanabaisha mnyororo mzima wa tasnia hiyo katika eneo maalumu ndani ya uwanja litakalopewa jina la “Mtaa wa Alizeti”


Aidha amesema kuwa ,kutakuwa na mada na maelezo maalum ya umuhimu kuhusu uzalishaji wa alizeti, matumizi ya mbegu bora na maandalizi stahiki ya mashamba. 


Kongamano la zao la Mtama


Mtama ni zao linalolimwa katika Kanda hii kwa miaka mingi kutokana na kustahimili hali ya hewa ya ukanda huu na hivyo kuchangia katika usalama wa chakula. Kwa sasa mtama sio zao la kukabiliana na njaa tena bali limegeuka kuwa zao zuri la kibiashara.


Amesema Mtama unatumika katika uzalishaji wa unga wa lishe, malighafi katika viwanda vya kutengeneza bia na pia lina uhitaji mkubwa nje ya nchi katika nchi za Burundi, Rwanda na Sudani.


Katika Mtaa wa mtama wananchi na wadau watapa fursa ya kufahamu nafasi ya zao hili katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na wa mikoa ya Dodoma na Singida.


Aidha, wakulima wataunganishwa na wanunuzi ili kupata soko la uhakika kwa kuwa wadau wote katika mnyororo wa uzalishaji na usindikaji watakuwepo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI