Na Matukio Daima App, Zanzibar.
CHAMA Cha ACT Wazalendo kimesema kitapitia mikataba yote ya uwekezaji na ujenzi endapo watashika madaraka mwaka 2025 na viongozi au watendaji watakaohusika na ufisadi au ubadhilifu watafunguliwa mahakamani.
Hayo yameelezwa na mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Ismail Jussa Ladhu alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika uwanja wa Chwaka Mkoa wa kusini Unguja.
Aidha amesema serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ipo katika hatari ya kufilisiwa mali zake baada ya kushtakiwa na kampuni ya Pennyroyal resolt kutakiwa kulipwa shilingi tirioli 2.5 baada ya kuifutia umiliki wa ardhi kampuni hiyo.
Akizungumzia miradi ya ujenzi wa barabara amesema kuna kampuni moja kutoka uturuki imekuwa ikipewa kazi ya ujenzi bila ya kutangazwa zabuni jambo ambalo ni kinyume na sheria ya dhabuni na ushindani zilizopitishwa na baraza la wawakishi Zanzibar.
Kuhusu ujenzi wa uwanja wa amani amesema kuna ufisadi mkubwa umefanyika kutokana na matumizi ya shilingi bilioni 51 kwa uwanja unaochukuwa watu 12,000 wakati ukarabati kama huo katika uwanja wa benjamani mkapa unatarajiwa kutumia shilingi bilioni 31.
Chama cha act wazalendo kinatarajia kukamilisha mikutano yake ya hadhara 12 iliyofanyika unguja na pemba ikiwa ni awamu ya kwanza tangu mikutano ya hadharak urughusiwa na rais wa Tanzania Samia suluhu Hassan baada ya kuzuwiwa kwa muda wam iaka saba.
0 Comments