Header Ads Widget

DC MKINGA ATAKIWA KUSHUGHULIKIA MIRADI YENYE UKAKASI.


 Na Mbaruku Yusuph-Matukio Daima APP, Mkinga.


MWENYEKITI wa chama cha mapinduzi mkoa wa Tanga Rajabu Abdurahman amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Mkinga kufuatilia matumizi sahihi ya fedha za ujenzi wa shule ya Sekondari ya  Kigongoi na zahanati ya Matemboni na hatua za kisheria zichukuliwe kwa ubadhirifu utakaobainika.


Mbali na agizo hilo pia amewaagiza watumishi wa Serikali kutimiza wajibu wao wakati wa kusimamia miradi ya maendeleo kwa maslahi ya wananchi wanaokabiliwa na kero mbalimbali.


Kauli hiyo ameitoa wakati wa ziara yake Wilayani humo wakati alipokuwa akikagua miradi ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kigongoi itakayogharimu Shs Mil 670 Zahanati ya Kijiji cha Nzigi Mwagogo uliyogharimu Shs Mil 67 na  ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa kwenye shule ya msingi mtundani ambayo yamejengwa kwa nguvu za wananchi na Serikali.


Aidha alisema mbali ya jitihada hizo za wananchi katika miradi hiyo ambayo imekwama kutokana na kukosekana kwa fedha za umaliziaji na amewaahidi wananchi katika maeneo hayo kukutana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga ili kuona hatua gani inaweza kutumika ili miradi hiyo iweze kumalizika.


Rajabu alisema wananchi wanaendelea kuteseka kwa kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya afya na elimu kutokana na kutokumalizika kwa miradi hiyo ambayo dhahiri inaonekana imekosa msukumo wa watendaji katika swala zima la usimamizi.


"Nilichogundua katika miradi hii muhimu kwa maslahi ya wananchi ni msukumo wa watendaji wetu lakini ninaimani kwa ushirikiano na Mkuu wa Mkoa wetu mwaka huu fedha zinapatikana ili wananchi waanze kunufaika"Alisema Mwenyekiti huyo.


Rajabu ambae pia ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa alisema ilani ya CCM na Sera ya Serikali ni kuhakikisha kila Kijiji kunajengwa Zahanati na kila kata kujengwe kituo cha afya ili kuwapunguzia adha wananchi kupata huduma hiyo kwa urahisi.


Aidha alisema mbali na swala hilo la Zahanati lipo tatizo la matumizi mabaya ya fedha za Serikali katika ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kigongoi sambamba na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mtundani ambao wanatumia muda mrefu kutembea jambo ambalo linawapotezea ari ya kusoma na ni hatari kwa maisha ya watoto hao.

"Nimesikia hapa toka kwa Mbunge wetu kwamba watoto wanatembea zaidi ya km kumi hii ni hatari sana lazima tuchukue hatua shule zijengwe kila mahali ili tuwapunguzie adha ya kutembea umbali mrefu watoto wetu"Alisema.


Mbunge wa Wilaya ya Mkinga Dastan Kitandula alikiri ujenzi wa miradi hiyo mitatu imechukua muda mrefu kumalizika kutokana na changamoto ya kifedha na migogoro ya wananchi na kumuomba Mwenyekiti huyo aweke msukumo ili miradi hiyo iweze kukamilika na iweze kutumiwa na  wananchi wa Kijiji hicho .


Kitandula alisema katika swala la shule yapo maeneo mengi Wilayani humo ambayo watoto wanatembea umbali mrefu takriban km kumi kufuata elimu ya msingi na Sekondari jambo ambalo kwa namna moja au nyingine linawathiri watoto hao.


Kwa uoande wa Diwani wa kata ya Manza Kadir Ramadhani alisema shule hiyo ya Mtundani ilikuwa na madarasa mabovu ambayo yalikuwa hatarishi kwa wanafunzi ambapo waliomba kibali kwa Mkurugenzi ili yavunjwe kabla hayajaleta madhara kwa wanafunzi.


Ramadhani ambae ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mkinga alisema wanachi waliamua kutumia nguvu zao kujenga madarasa hayo matatu na Halmashauri iliwaunga mkono madarasa mawili kuyamalizia.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI