WAZIRI Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Baraza la Chakula Nchini Mizengo Pinda ameiomba serikali kupitia wizara ya kilimo kuhamasisha wakulima kulima kilimo Cha umwagiliaji na kuachana na kilimo Cha kutegemea mvua ili kupata mavuno mengi zaidi katika kukuza Uchumi wa Nchi.
Pinda ameyasema Leo jijini hapa wakati wa uzindua wa Mkakati wa Sustainably Growing Afric's Food System (SGRA) wa 3023_2027 .
Pinda mesema Nchi ya Israel imepiga hatua katika kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia maji ya bahari hivyo Ni muda. Sasa wa Nchi ya Tanzania kutumia Kilimo Cha. Umwagiliaji.
" Nilikuwa najiuliza Sasa sisi Tanzania tunakwama wapi Kama hahari na mito tumejaaliwa Kwanini tusifanye kilimo Cha umwagiliaji kupitia bahari yetu na mito yetu ," alisema Waziri Mstaafu
Sambamba na hayo alimtaka Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo kuhakikisha wakulima wote nchini was nalima kwa tija ikiwa ni pamoja na kuachana na kilimo Cha Mazoea.
Katika hatua nyingine aliitaka wizara ya kilimo kuhakikusha kila Afisa ugani anapewa idadi ya kaya ili aweze kusimamia .
"Hata katika Kijiji kimoja kuwepo na .aafisa ugani wawili kukingana na idadi husika," Amesema Waziri Pinda.
Kwa Upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema mkakati wa serikali ni kuhakikisha wanaweka mkazo katika kilimo Ufugaji na Uvuvi kwani huko ndipo kwenye Watu wengi zaidi.
Waziri Ulega amesema kwa muda mrefu Taifa Kimekuwa likisumbuka na tatizo la utapiamlo na kusahau protini ya mimeq na wanyama ndio jawabu na suruhusho kwenye utapiamlo.
Aidha Amesema kwa Upande wa wakulima wamekuwa wakikabiliwa na Changamoto ya masoko lakini ukweli ni kwamba masoko makubwa kwa mkulima ni mfugaji .
" Tanzania tumekuza tukipeleka mabaki mengi ya kilimo mazao ,mashudu nje ya nchi na yamekuwa yakitupatia fedha nyingi za kigeni ,"amesema Waziri Ulega.
Naye Country manager Vianey Rweyendela Amesema mkakati huo umejikita katika maeneo manne ambayo ni upatikanaji wa mbegu Bora, Uwezeshaji wa taasisi za serikali, Matumizi Bora ya ardhi pamoja na masoko shirikishi.
0 Comments