Header Ads Widget

"ALIEJIKATA UUME ANAO UWEZO WA KUPATA MTOTO"_ DKT. MAKALLA




NA HADIJA OMARY LINDI.....


Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Lindi Sokoine Dr.Alexander Makalla amesema kijana Simon aliyejikata uume wake anao uwezo wa kupata mtoto endapo anauhitaji huo.



Dr Makalla ametoa kauli hiyo kwa waandishi wa habari waliofika hospitalini hapo kufahamu hali ya kijana huyo ambapo amesema kutokuwepo kwa uume hakuwezi kumuathiri katika maisha yake ya kawaida,anaweza kupata hisia hisipokuwa atakosa kushiriki tendo la ndoa ingawa anaweza kupata mtoto bila kufanya tendo hilo.



Amesema mfumo wa uzazi umegawanyika katika sehemu kuu mbili(mfumo wa uzazi wa ndani na nje)na kwa mwanaume mfumo wa uzazi wa nje unahusisha uume na korodani ambapo korodani zinazalisha mbegu za kiume na uume ni kama nyenzo ya kuchukua mbegu za kiume na kuweka  kwenye uke,na kwa sasa kuna uwezekano pia wa kuvunwa mbegu za kiume kwake na kupandikizwa mwenza wake na kupata  mtoto kama kawaida kwakua mbegu za kiume bado zinaendelea kuzizalishwa.



Kuhusu kupandikiza uume ameeleza kwamba anaweza kufanya hivyo kwa kuwekewa uume wa bandia endapo kama atakuwa na uwezo kifedha kumudu kupata huduma hiyo jambo litakalomsaidia kuweza kushiriki tendo la ndoa ingawa hatofikia hisia kwa asilimia mia moja kama uwezo wake wa awali .



Akieleza hali ya Mgonjwa,amesema kutokana na tatizo lake la afya ya akili ,licha ya kuanza kuongea na kutembea lakini bado wauguzi na wataalam wa magonjwa ya akili wanaendelea na matibabu kuhakisha afya yake inakaa sawa na kwamba hawawezi kumruhusu mgonjwa huyo kurudi nyumbani mapema kwa kuhofia akirudi nyumbani anaweza kuendelea kujidhuru zaidi kwani awali alipohojiwa juu ya kilichotokea alikiri kujidhuru mwenyewe kwa kutumia kisu gutu akidai kuwa hayo ni MAELEKEZO  ambayo amekuwa akipewa kutoka juu na kwakua yeye ni mfalme mwaminifu  anatekeleza maagizo hayo.



Ameongeza kuwa wakati huu amewekewa mpira kwaajili ya kumsaidia kupata haja ndogo na kupona majeraha yake vizuri asipate maambukizi kwenye kidonda na baada ya wiki mbili mpira huo utatolewa na hivyo atakuwa yupo sawa.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI