Header Ads Widget

RAIS DKT MWINYI KUKIMBIA KM 5 MBIO ZA TIGO ZANTEL

 


NA THABIT MADAI ZANZIBAR: HABARI ZANZIBA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi na anatajiwa kukimbia umbali wa Kilimita 5 katika Msimu wa Tatu wa Tigo Zantel Zanzibar Intarnational Marathon ambayo inatarajiwa kufanyika Mwezi wa 10 Mwaka huu.

Msimu wa Tatu wa Mbio za Tigo Zanzibar International Marathoni imekuja na vitu mbalimbali ikiwemo Mbio maalum za Watoto na Vijana pamoja na kuongeza zawadi mbaimbali kwa Washindi wa Mbio hizo.

Akizungumza wakati wa Uzinduzi Rasmi wa Mbio hizo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar Tabia Maulid Mwita ameeleza Serikali kupitia Wizara itaendelea kuunga mkono juhudi za kuendeleza Michezo mbalimbali ambayo itatoa fursa za Ajira kwa Vijana.

"Serikali kupitia Wizara inaendelea kusimamia Sera ya Michezo kwa wote ambapo Michezo

Mapema, Meneja wa Kanda wa Tigo Zantel Zanzibar Mohammed Waqid ameeleza kuwa lengo la kuendeleza Mbio hizo kutangaza utalii wa Zanzibar na kuimarisha Afya za Vijana mbalimbali.

"Tunaamini kuwa Mbio hizi zinachochea ukuaji wa Utalii Visiwani hapa pamoja na kumarisha Afya ya Vijana mbalimbali,"

Mapema Mratibu wa Mbio hizo Hassan Mussa Ibrahim ameleza kuwa Msimu wa Tatu wa Mbio hizo umeboresha zawadi kwa Washindi pamoja na aina ya uendeshaji wa Mbio hizo.

"Malengo yetu kufanya Mbio hizi kuwa na washiriki wengi zaidi kutoka kila kona Dunia na kuongeza idadi ya Watalii wanaotembelea Zanzibar," alieleza.

Kamati kuu ya mbio hizo  ilitangaza rasmi kuingia mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya huduma za mitandao ya simu ya Tigo & Zantel, kwa mkataba mnono wa Billion 1.5

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI