Header Ads Widget

WADAU WATAKA VIWANGO RAFIKI TOZO MPYA ZA TPA

 


Mkurugenzi wa udhibiti wa usafiri wa majini TASAC Deogratius Mukasa  (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchakato wa ukusanyaji maoni ya wadau wa bandari kuhusiana na mapendekezo tozo mpya yaliyowasilishwa na Mamlaka ya usimamizi wa bandari (TPA)

Na Fadhili abdallah,Kigoma 

WADAU wa bandari katika mwambao wa ziwa Tanganyika mkoani Kigoma wameitaka Shirika la Wakala wa meli nchini (TASAC) kuweka viwango rafiki za tozo za huduma za bandari ili kuwezesha kuondoa tozo kubwa zinazopigiwa kelele na wadau na wananchi wanaotumia bandari za ziwa Tanganyika.

Hayo yamesemqa kwenye mkutano wa siku moja wa wadau hao wa bandari  uliojumuisha watoa huduma mbalimbali katika bandari za ziwa Tanganyika wakitoa maoni na mapendekezo dhini  marekebisho ya tozo zilizowasilishwa na uongozi wa Mamlaka ya usimamizi wa bandari  (TPA)

Mmoja wa wadau hao Brian William, wakala wa forodha katika Mwambao wa ziwa Tanganyika alisema kuwa kwenye mapendekezo yao wameomba  kupunguzwa kwa  viwango vya tozo ambazo  zimekuwa mzigo kwa wasafirishaji wa shehena na wadau wanaotumia bandari za ziwa Tanganyika kupitia Bandari ya Dar es salaam wakieleza kuwa tozo hizo bado ni kubwa na zinakimbiza wateja.


William alitoa mfano wa tozo ya ushushaji na upakiaji wa kontena katika bandari ya Dar es Salaam ambayo hutozwa dola 120 wakati kontena kama hilo hutozwa dola 140 kwa bandari ya Kigoma.

Naye Dunia Shakuru Wakala wa meli kutoka kampuni ya DS SALUTA & SONs Ltd alisema kuwa zipo tozo ambazo hazipaswi kuwepo na zinapaswa kuondolewa kabisa ikiwemo tozo ya shilingi 600 wanayotozwa wananchi wanaosafiri na vyombo mbalimbali kwenye ziwa Tanganyika wakati wanasafiri ndani ya nchi na tozo hiyo haina maana yeyote.

Kufuatia maoni hayobSHIRIKA la Uwakala wa Meli nchini (TASAC) limesema kuwa litazingatia Maoni yaliyotolewa na wadau wa usafirishaji   majini mkoani Kigoma kuhusiana na maombi ya mamlaka ya usimamizi wa bandari nchini (TPA) kupitia na kupanga upya tozo mbalimbali katika bandari zake nchini na kwwmba tozo zitakazopitishwa zitazingatia uhalisia wa utoaji huduma kwa pande zote.

Mkurugenzi wa udhibiti wa usafiri kwa njia ya maji kutoka TASAC,  Deogratius Mukasa alisema hayo akihitimisha mkutano wa siku moja wa wadau wa bandari   akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Kaimu Mshindo Mkeyenge.

Mkurugenzi huyo  alisema kuwa ukusanyaji huo wa maoni utaendelea hadi Julai 20 mwaka huu na baada ya hapo maoni ya wadau wa bandari yaliyokusanywa kulingana na mapendekezo ya TPA yaliyowasilishwa  kwenye vikao vya bodi  za  TASAC ili kuweka uwiano wa viwango vinavyokusudiwa kulingana na hali halisi ya huduma inayolengwa

Hata hivyo alisema kuwa kikao hicho kimeonyesha kutimiza malengo yake kutokana na walengwa kukubaliana na baadhi ya mapendekezo yaliyowasilishwa na TPA lakini pia wakitaka baadhi ya tozo kupunguzwa na nyingine kuondolewa kutokana na kuwa mzigo kwa wadau, wasafirishaji shehena na wananchi.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI