Header Ads Widget

MBUNGE AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA BODABODA

Na , Matukio daima media,Mbarali

MBUNGE wa Jimbo la Mbarali , Francis Mtega amefariki dunia baada ya kupata ajali ya pikipiki aliyokuwa akiendesha kugongana uso kwa uso na Powertiler na kupelekea umauti kumfika.


Ajali hiyo imetokea kata ya Ihai wilayani Mbarali mkoani Mbeya ambapo Mbunge huyo alikuwa akiendesha kuelekea shambani kwake ambapo nyuma alipakia mifuko kwa ajili ya kwenda kuvuna mpunga shambani kwake.


Akizungumza na matukio daima ,Diwani wa kata ya Kongolo mswiswi ,Elia Bange amesema kuwa baada ya ajali hiyo kutokea majeruhi alikimbizwa hospital  ya Chimala  na kuwa kabla ya kupatiwa matibabu  alifariki katika hospitali ya mission ya Chimala


Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mbarali ,Twalibu Lubandamo amekiri kutokea kwa kifo cha Mbunge  Francis Mtega kilichosababishwa na pikipiki aliyokuwa akiendesha wakati akielekea shambani kwake kata ya Ihai .


"Hivi sasa tupo njiani tunaelekea hospitali ya wilaya ya wilaya kwa ajili ya kwenda kuhifadhi mwili wa Mbunge wetu wakati tukisubiri taratibu zingine"amesema Mwenyekiti huyo wa halmashauri.


Mkuu wa wilaya ya Mbarali ,Col.Denis Mwila amekiri kutokea kwa ajali hiyo ambapo anesema tukio hilo limetokea majira ya 15.30  alasiri eneo la kibaoni ambapo marehemu mtega alikuwa akiendesha pikipiki aina ya Boxer  yenye namba MC  573 CGT .


Amesema kuwa Powertiler aina ya  kubota iliyokuwa ikiendeshwa na  Alex Musa (18) mkazi wa kibaoni ilikuwa ikitoka kapunga ilimgonga  mwendesha pikipiki huyo ambaye ni mbunge wa Jimbo la Mbarali na kusababisha umauti.


Aidha Col.Mwila amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo uzembe wa opareta wa Powertiler kwa kutochukua tahadhari kwa watumiaji wengine wa barabara.


Mtuhumiwa wa Powertiler amekakatwa yupo kituo cha polisi Chimala.


Hata hivyo marehemu Mtega licha ya kuwa Mbunge pia alikuwa Mwenyekiti wa parokia ya Chosi kata ya Chimala wilayani Mbarali.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI