Na Ibrahim Kunoga, Tanga.
Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Kasim Majaliwa kasimu ameipongeza kampuni ya Gbp inajushughulisha na uuzaji na usambazaji wa mafuta kwa kanda ya kaskazini
Waziri mkuu ametoa pongezi hizo baada ya kutembelea kampuni hiyo wakati wa ziara yake ya siku moja jijini Tanga iliyolenga kutembelea maendeleo ya upanuzi wa bandari ya Tanga.
Amesema uwekezaji uliofanywa na kampuni hiyo ni mkubwa kwani matenki yaliyopo yanaweza kupokea mafuta moja kwa moja kutoka bandari ya Tanga na kuhifadhi.lita zaidi ya milioni 200.
Katika ziara hiyo Majaliwa amesema huo ni mkakati wa Rais Samia Suluhu Hassan wa kuendeleza uchumi wa nchi.
Amesema wakati serikali inaongeza uwezo wa kusimamia meli bandarini watahakikisha uwekezaji huo unaleta tija kwa wakazi wa Jiji la Tanga ikiwemo vijana kupata ajira.
Awali akitoa taarifa kuhusu hifadhi ya matenk ya Gbp Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Badar Sood amesema ujenzi wa matank hayo ulianza mwaka 2002 yakiwa na uwezo wa kuhifadhi lita milioni 25 huku wakipokea meli zenye uwezo wa lita 6000 tu
0 Comments