Header Ads Widget

MAMA MARIAM MWINYI AMESEMA NI LAZIMA KUSIMAMIA MAADILI YA WATOTO

 



NA MATUKIO DAIMA APP, ZANZIBAR 

MKE wa Rais wa Zanzibar mama Maryam Mwinyi, amesema katika kuyasimamia maadili ni vyema kuwekeza kwa vijana na watoto wadogo katika kuwapatia stadi za maisha na kuwakinga na vitendo vya udhalilishaji.

Mama Mwinyi alieleza hayo katika hotuba yake iliyosomwa na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Mgeni Hassan Juma katika mkutano wa Chama cha Wanawake Wamiliki wa skuli na Vyuo vya Kati Tanzania (TAWASCO) uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Abla Mtoni.

Alisema lengo hilo ni kuwawezesha kubaini mapema mazingira hatarishi ili kujikinga na kujilinda wao wenyewe na kutokufanya na kufanyiwa udhalilishaji.

Aidha alisema ni lazima kujitahidi kuandaa jamii isiyo na udhalilishaji kwa kutumia ujuzi, umahiri, hekima elimu na maarifa waliyonayo katika kukabiliana na tatizo hilo ili hatimae maadili yenye kuzingatia utu na kuheshimiana yachukue nafasi yake kama ilivyokuwa hapo awali.


Alisema kwa wanafunzi suala hilo linazingatia kufikia mtaala kujenga misigi ya upatikanaji wa elimu,nyenzo na miongozo mbalimbali ya kufundishia.

Hata hivyo, alibainisha kuwa ushirikishwaji wa watoa huduma katika kuunga mkono juhudi za serikali ni suala muhimu sana.

Alisema suala la kuimarisha miundombinu ya elimu ni miongoni mwa kiashiria muhimu katika kufikia utoaji wa elimu bora Tanzania na duniani kote.

Alisema anaamini mkutano huo utawawezwesha kujua mafanikio changamoto na namna ya utatuzi wake kwa kuweka maazimio ya utekelezaji wakiwa na lengo la kuona taasisi hiyo inazidi kupiga hatua zaidi ili kufikia malengo iliyojiwekea.


“Mkusanyiko huu itakuwa darubini yua kumuruka mbali kuhakikisha yanapatikana matokeo chanya ya dhamira na malengo mliojipangia,” alisema.


Aliwapongeza TAWASCO kwa uthubutu wa kuanzisha umoja huo muhimu katika tasnia ya elimu nchini.


Alisema hatua hiyo inaonesha wazi kuwa wanawake wanaweza kujipanga kuchangia maendeleo ya nchi.


Hivyo aliwapa moyo kutokata tamaa kutokana na changamoto zinazowakabili kwani umoja huo una malengo mazuri na manufaa na faida kubwa sio kwa wanawake tu bali kwa jamii yote ya watanzania.


Hivyo, aliahidi kuzichukua changamoto hizo na kuziwasilisha kunapohusika ili ziweze kufanyiwa kazi.


“Serikali zetu zote mbili ya SMZ na SMT ni sikivu zinathamini na kutambua kazi inayofanywa na umoja wenu hivyo nina imani kero zenu zitazingatiwa na kupatiwa ufumbuzi,” alisema


Mama Maryam, aliahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha wanafikia malengo ya kuanzishwa kwa umoja huo ambao kwa hakika ni kielelezo muhimu cha jitihada za wanawake wa Tanzania katika kusimamia maadili, malezi na kuelimisha jamii hususan watoto.


Hata hivyo alikubali ombi la kuwa mlezi wa TAWASCO na imani yake kumalizika kwa mkutano huo kutatoa mwanga na dira ya kuzidi kupiga hatua za maendeleo katika kutimiza jukumu lao kama wanawake la kuelimisha jamii mambo mema na kusimamia maadili hasa ya watoto na familia kwa ujumla. 


Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ali Abdulgulam Hussein, aliupongeza umoja huo kuendeleza mashirikiano ambayo uanatokana na kuimarika kwa Muungano kwa pande zote mbili na kuahidi kuwa wizara ipo tayari kushirikiana na chama hicho kuhakikisha wanakwenda kutatatua changamoto mbalimbali zinazowakabili sekta binafsi ambao wamewekeza katika sekta ya elimu.


Aliwaomba watoto wa kike kuhakikisha wanajikinga na vitendo vya udhalilishaji kwani taifa linawekeza kwa mtoto wa kike ili dunia iende salama.


Naye Mwenyekiti wa chama hicho, Mercy Sila, alisema mkutano huo utatoa elimu kwa wanafunzi wa skuli za serikali na binafsi juu ya namna ya kujikinga, kujilinda na vitendo vya ukatili na kuzunguka katika mikoa yote ya Tanzania bara na Zanzibar hasa katika maeneo ambayo yameonekana kushamiri kwa vitendo hivyo.


Walimuahidi mama Maryam kuunga mkono juhudi zake za malezi na kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu nchini na skuli na vyuo vitakuwa mfano wa kuigwa na taasisi nyengine za elimu Tanzania.


Alibainisha kuwa wadau wa taasisi yao wanatoa mchango mkubwa katika njanja za kiuchumi na kijamii kwani hivi sasa nchi ina taasisi zaidi ya 1,000 zinazojishughulisha na utoaji wa elimu na mafunzo na ambazo zinamilikiwa na wanawake ambapo kati ya hao ambao wamejiunga ya TAWACSO ni 200.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI