Header Ads Widget

UJENZI WA SHULE YA BILIONI 4.1 WANGING'OMBE WAMVURUGA RC NJOMBE

 



Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Kusuasua kwa ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya wasichana ya masomo ya Sayansi kidato cha Tano na sita katika kijiji cha Usalule ambayo ilipaswa kukamilika mwezi  septemba mwaka huu kumeonekana kumkera  mkuu wa mkoa wa Njombe na kulazimika kuagiza uongozi wa wilaya ya Wanging'ombe kusalia katika eneo la mradi kujadili hatma ya ujenzi huo.


Hatua hiyo imekuja baada ya mkuu wa mkoa kutembelea na kukagua ujenzi wa shule hiyo ambayo ilipewa fedha kiasi cha shilingi bilioni 4.1 tangu mwaka jana mwezi agosti lakini hadi sasa majengo mengine likiwemo la utawala hayajaanza hata kuchimbwa msingi.


Awali afisa elimu mkoa wa Njombe Nelasi Mulungu amesema Lengo la serikali ilikuwa ni kupokea wanafunzi mwezi wa Nane mwaka huu lakini kutokana na kusua sua kwa ujenzi wa shule hiyo wamelazimika kuwapeleka katika shule nyingine.


Aidha Wakandarasi wa mradi huo akiwemo Samuel Mhelela Joseph Nyikonde na Mariam Sangalawe wamesema kilichochelewesha utekelezaji wa mradi huo ni kuchelewa kupelekwa kwa maji katika eneo la mradi pamoja na upatikanaji wa vifaa vingine.


Sababu hizo zimeshindwa kumshawishi mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka ambaye amelazimika kuagiza uongozi mzima wa wilaya  ya wanging'ombe chini ya mkuu wa wilaya hiyo Claudia Kitta kusalia kwenye mradi huo kujadili namna ya kutekeleza mradi huo kwa wakati.



Kwa upande wao wakazi wa wilaya ya Wanging'ombe akiwemo Eloniki Kadege na Okoka Msombe nao wameshangazwa na kusua sua kwa ujenzi wa shule hiyo ilihali fedha zilitolewa tangu mwaka jana.


Mradi wa shule mpya za sekondari za wasichana wa kidato cha tano na sita kwa masomo ya sayansi ulipata fedha toka serikali kuu kwa kila mkoa ambapo mkoa wa Njombe uliamua kuanza ujenzi wa shule hiyo katika kijiji cha Usalule wilaya ya Wanging'ombe ambako uongozi wa kijiji ulitoa ekari 105 bure.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI