SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imeendelea kuimarisha na kudhibiti huduma za usafiri majini, sambamba na kuhakikisha kuna ushindani sawia miongoni mwa watoa huduma .
Hayo yemesemwa leo jijini Dodoma Julai 27, 2023 na Mkurungezi wa Shirika hilo TASAC Kaimu Mkeyenge wakati akielezea utekelezaji wake na muelekeo wa Mwaka wa2923/24
Amesema Shirika hilo limeendelea kufanya ufuatiliaji, tathmini na kutoa maelekezo kuhusu utekelezaji wa vigezo na viwango vya ubora wa huduma (performance standards and Benchmarks) kwa watoa huduma za bandari na usafiri majini;
Pia ameeleza Shirika limeendelea Kuratibu maombi ya tozo za usafiri wa meli katika Maziwa (Victoria na Nyasa) na kuhakikisha viwango vya tozo vinavyotumika haviathiri ushindani wa kibiashara;
"Katika Kuendelea na zoezi la urasimishaji wa bandari bubu Tanzania bara bandari bubu kumi na tatu (13) zilizowasilishwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) kwa ajili ya urasimishaji zilikaguliwa na kufanyiwa tathmini ya kina kwa kushirikiana na TPA, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC),''amesema
Na kuongeza " Bandari bubu kumi zilionekana kukidhi vigezo hivyo na kupendekezwa kwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) (WUU-U) kwa ajili ya kurasimishwa kwa mujibu wa sheria," Amesema Mkurungezi huyo
Aidha amesema ,waendeshaji wa zilizokuwa bandari bubu binafsi tano (05) za Mwanza ambazo ni miongoni mwa zilizokuwa bandari bubu ishirini (20) zilizorasimishwa kupitia Tangazo la Serikali (GN) namba 293/2022 wamepewa leseni za uendeshaji huku TPA wakielekezwa kusimamia kwa karibu bandari kumi na tano (15) zilizobakia.
Katika kutimiza lengo hili la kimkakati; Shirika limeendelea kusimamia usalama wa vyombo vya usafiri majini kwa kufanya ukaguzi wa meli kubwa na vyombo vidogo vya majini .
Amebainisha kuwa ,Shirika limekuwa likifanya kaguzi za usalama kwa meli kubwa zibebazo tani 50 au zaidi ili kuhakikisha kuwa ni salama na zinaendeshwa na mabaharia wenye sifa katika mikoa ya Dar es Salaam,Mtwara, Tanga, Mwanza, Kagera, Kigoma na Mbeya ambapo katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Juni, 2023, Shirika lilifanya jumla ya kaguzi za meli kubwa 288 ambapo kaguzi 165 zilikuwa za meli zakigeni na kaguzi 123 zilikuwa meli za ndani.
MPANGO MKAKATI WA UTEKELEZAJI KATIKA MWAKA WA FEDHA 2023/24
Kuboresha udhibiti wa huduma za usafiri na usafirishaji kwa njia ya maji nchini sambamba na kuweka ushindani ili kuhakikisha huduma za usafiri majini zinakuwa endelevu.
Kuimarisha Usalama na Ulinzi kwa usafiri kwa njia ya maji sambamba na Udhibiti wa Uchafuzi wa Mazingira utokanao na usafiri wa Meli.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa
Amesema Serikali inataka kushirikiana na sekta binafsi kuendesha Bandari, mikataba na watakaoendesha bado haijasainiwa.
"Sasa hivi ndio wataalamu wako mezani kuzungumza kuhusu mikataba, muda na gharama," Amesema
Na kuongeza "Lakini hakuna Bandari iliyouzwa, wataalamu watakapokamilisha majadiliano tutaangalia maslahi yetu yako wapi na maoni yanayotolewa na Watanzania yatazingatia," .
Hata hivyo ameeleza kuwa ,Serikali iko macho wakati wote kuhakikisha maslahi ya Watanzania yanalindwa.
0 Comments