Na Gift Mongi MATUKIODAIMA APP MOSHI.
Ukiwa ni utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi (2020-2025)katika kuhakikisha wananchi wanaondokana n
a matumizi ya kuni kama sehemu ya nishati katika jimbo la Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro tayari wananchi wake wameanza kujengewa uelewa ukiwamo matumizi ya gesi.
Kutokana na kampeni hii huenda wananchi walio wengi wataenda kuachana na matumizi ya kuni na mkaa na badala yake kutumia nishati mbadala katika kuhifadhi mazingira.
Hata hivyo kwa muda mrefu sasa baadhi ya viongozi hususani katika mkoa wa Kilimanjaro wamekuwa wakilalamimia ukataji wa miti hovyo kama sehemu ya nishati ikiwemo kuni na mkaa.
JE NINI KIFANYIKE?
Serikali ya sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan imejikita zaidi katika kutoka mazingira na sanjari na hilo kuona kwamba wananchi wanaondokana na matumizi ya kuni pamoja na mkaa ambavyo kwa pamoja vinachangia uharibifu wa mazingira.
Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro Prof Patrick Ndakidemi anasema tayari amepokea mitungi ya gesi ipatayo 100 lengo likiwa ni kuhamasisha wananchi wake kuachana na matumizi ambayo sii rafiki Kwa mazingira
'Tunamshukuru sana mheshimiwa Rais Dkt Samia kwa kuendelea kuhamasisha matumizi sahihi ya nishati leo nikabidhi cheti cha makubaliano ya ununuzi wa mitungi 100 ya gesi'anasema
Hata hivyo kwa mujibu wa mbunge huyo ni kuwa serikali imetenga fedha katika bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 hususan katika wizara ya nishati na lengo na kuwainua wananchi kwa kutumia nishati mbadala.
JE NI UPI MTAZAMO WA WASAMBAZAJI WA GESI?
'Kipekee tunashukuru kupata nafasi ya kutoa huduma hii kwa wakazi wa jimbo la Moshi Vijijini na hakika tunasitiza matumizi ya nishati mbadala katika kuokoa mazingira'anasema Haleluya Kagero ambaye ni afisa masoko wa taifa gesi mkoa wa Kilimanjaro.
Anaongeza kuwa matumizi ya nishati ya gesi hususan majumbani ikawa ni sehemu ya suluhisho la kudumu katika upatikanaji wa nishati na kuwa wananchi walio wengi wkitumia nishati hiyo itakuwa ni njia mojawapo katika kutunza mazingira
JE NI YAPI MAONI YA WANANCHI?Baraka Ollomi mkazi wa Kibosho Kirima anasema kupatikana kwa nishati hiyo huenda kukawa ni njia mojawapo kuponyesha mazingira ambayo itaenda sanjari na kupunguza matumizi ya nishati ya kuni na mkaa kama sehemu ya nishati.
'Tunashukuru kwa mtizamo huu wa serikali katika kutukwamua katika hii hali tuliopo sasa nakutepeleka kutumia nishati ya gesi hii inaenda kutujenga upya na kuachana na matumizi ya gesi ama kuni ambayo yamekuwa yakiharibu mazingira'anasema
Mwisho.
0 Comments