NA HADIJA OMARY LINDI...
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga amewaagiza wakala wa Barabara mijini na vijijini TARURA Wilaya ya Lindi kuwasimamia wanaotekeleza miradi mbali mbali ya Barabara wilayani humo kujenga wa ubora ili barabara hizo ziweze kutumika kwa muda mrefu
Ndemanga ametoa wito huo mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea miradi 7 ya barabara inayoendelea kujengwa na kivuko 1 ambacho kimekamilika kilichojengwa katika kata ya Mchinga Manispaa ya Lindi, akiwa ameambatana na kamati ya usalama na viongozi wa chama cha Mapinduzi wa Wilaya hiyo
Ujenzi huo wa barabara unaoendelea ni barabara ya Mahiwa-Namangale,Nyengedi ,mnara hadi Rondo forest km 5 kwa kiwango cha lami na Nangaru Milolo kwa kiwango cha changalawe
Ndemanga alisema ili miradi hiyo iweze kuleta manufaa yaliyokusudiwa ni muhimu kwa wakandarasi kujenga katika ubora ili itumike kwa muda mrefu.
Hata hivyo Ndemanga pia ameagiza barabara ya Nangaru inayojengwa na Mkandarasi Malaika Building and Civil Works Ltd kuongeza kasi na kuhakikisha anachonga vizuri milima iliyopo kwenye barabara hiyo ili ikawe msaada kwa wananchi wanaotaka kufika barabara kuu ya kwenda Dar es salam.
Aidha amewataka Tarura washirikiane na halmashauri ya Mtama kuzitambua barabara ambazo zimefunguliwa ili zidajiliwe ziingie katika mpango.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Wananchi wa maeneo hayo akiwemo Asnati saidi mkazi wa Nangaru na Elias Ulomi wameishukuru Serikali kwa kuwa ujenzi wa barabara hizo utakapokamilika utarahisisha usafiri na usafirishaji wa mazao yao na kuwawezesha kuyafikia maeneo yenye huduma muhimu kama hospitali,masoko na shule.
Wakati wa ziara hiyo Meneja wa Tarura Wilaya ya Lindi Mhandisi Dawson Paschal amesema thamani ya miradi yote 7 ya barabara na kivuko 1 ni ni Bilioni 5.7 na kati ya hiyo km 5.7 inajengwa kwa kiwango cha lami na kwamba wanaendelea kuwasimamia wakandarasi kwa ukaribu ili ikamilike kwa wakati .
Mhandisi Dowson alisema kuwa wanazihamasisha Halmashauri za Wilaya hiyo kupima barabara zenye upana wa kutosha kuondoa changamoto wanazokutana nazo wakati wa ujenzi kama kuwepo kwa upana mdogo wa eneo la kujenga barabara hivyo kusababisha kushindwa kujenga njia ya watembea kwa miguu pia wananchi kudai fidia kwa uharibufu unaotokea wakati wa ujenzi.
0 Comments