Header Ads Widget

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MAADHIMISHO YA SIKU YA KUPAMBANA NA RUSHWA BARANI AFRIKA.

 


Teddy Kilanga,Arusha.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi,Dk Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuzindua Maadhimisho ya siku ya kupambana na rushwa barani Afrika yatakayofanyika jijini Arusha kuanzia julai 9 hadi 11,2023.


Akizungumza Waandishi wa habari,Mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongela amesema Rais Mwinyi atazindua maadhimisho hayo sambamba na kuongoza maandamano ya kupinga rushwa ambayo yataanzia katika Ofisi ya mkuu wa mkoa.


Aidha Mongela amesema siku ya kilele cha maadhimisho hayo,Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufunga maadhimisho hayo julai 11,2023.


"Lengo la maadhimisho ya siku hii ni kutoa nafasi kwa nchi wanachama juu ya kutafakari juhudi  za mapambano dhidi ya rushwa na kuchukua hatua stahiki kuboresha  kuhimarisha  mapambano hayo,"amesema Mongela.


Mongela amesema Sanjari na maadhimisho dhidi ya rushwa barani Afrika katika mwaka 2023 pia wanaadhimisha  miaka 20 ya utekelezaji wa mkataba  wa umoja wa Afrika wa kuzuia na kupambana na rushwa(AUCPCC) ambao ulisainiwa mwaka 2003.


Mkuu huyo amesema maadhimisho hayo yanatarajiwa kukutanisha  wadau mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania ambao watashiriki wakiwemo viongozi na watumishiwa Taasisi za serikali ,mashirika  ya umma pamoja na Wakuu wa mamlaka za kuzuia  na kupambana na rushwa za Afrika.


Ameongeza kuwa wengine ni pamoja na wanasiasa,wawakilishi wa mabalozi na Taasisi binafsi,viongozi wa dini,Vyombo vya Habari,Wajumbe wa AUABC na watumishi wa sekretarieti ya bodi hii.


Hata hivyo Mongela amewasihi wananchi kujitokeza katika matembezi hayo kama ilivyo desturi ya wakazi wa mkoa huu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI