Header Ads Widget

SHAZIA SHAFI :MTOTO WA KWANZA WA KITANZANIA KUANDIKA KITABU CHENYE KURASA NYINGI



Shazia Shafi, binti wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 12. Amezaliwa nchini Uingereza katika mji wa Reading na kuhamia Jiji la Abu Dhabi nchi za falme za Kiarabu akiwa na umri wa miaka miwili pamoja na wazazi wake Dkt Shafi Ayoub Mohammed na Bi Aziza Mohammed Saleh.


Shazia ni binti wa kwanza wa kitanzania mwenye umri mdogo kuandika kitabu kwa lugha ya kiingereza chenye kurasa zaidi ya mia . Alianza kuandika kitabu hiki akiwa na umri wa miaka 9 na kukikamilisha akiwa na umri wa miaka 10.



Kitabu hiki kinaitwa "REBORN", maana yake KUZALIWA TENA. 


Kitabu kina kurasa zaidi ya mia. Kitabu kinahusu kisa cha msichana  aitwae Kate.


Hapo mwanzo msichana huyu alikuwa katika familia ya kimasikini.Hali ya familia ikabadilika kiuchumi msichana huyu alipofika umri wa miaka 7. 


Mabadaliko haya yalimfanya msichana huyu kubadilika kitabia na muonekano katika jamii.


Msichana huyo alipata ajali ambayo  ni sababu ya kuleta mabadiliko katika maisha yake. Na hii ndio  sababu ya kitabu hiki kuitwa REBORN au KUZALIWA TENA.


Upatikanaji wa Kitabu


Kitabu hiki kinapatikana kwa hard copy katika tovutiza AMAZON na Publisher  AUSTIN MCKAULEY. 

Unaweza pia kununua copy ya electronic ya kitabu hiki kwa ku download kwa kindle kutoka ktk tovuti ya AMAZON.


Kwa  hapa Tanzania, kitabu hiki kinaweza kupatikana kutoka  *Elite Book Store* iliyopo pale Mbezi Beach maeneo ya Tangi Bovu

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI