Header Ads Widget

SERIKALI YAOMBWA KUTOA MIKOPO KWA WANAFUNZI WANAOENDA KUSOMA NJE YA NCHI




Mkurugenzi wa Taasisi inayowakilisha Vyuo Vikuu vya nje ya Nchi Tanzania (UAR) Tony Kabetha ameiomba Serikali  kutoa mikopo, kwa Wanafunzi wanaoenda kusoma nje ya Nchi ili kuwawezesha kufikia malengo yao pamoja na kuijenga Nchi yao kiuchumi.

Wito huo umetolewa  kwenye maonyesho ya 18 ya Elimu ya Juu,Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Nchini( TCU)  ambayo yanaendelea  katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.


Hata hivyo Kabetha anaeleza  kwamba Wanafunzi wamekua na kiu ya kwenda kusoma katika vyuo vya nje lakini wanashindwa kutokana na gharama kuwa kubwa, hivyo anaiomba  Serikali  kuwapa mikopo inayolingana na wanafunzi wanaosoma hapa Nchini ili waweze kwenda kusoma na kuweza kuja kuijenga nchi kiuchumi.


“Tanzania ni nchi inayoendelea hivyo inahitaji wawekezaji wengi wa tenkolojia, tunakaribisha wawekezaji ambao unakuta wamesoma kwenye vyuo hivihivi ambavyo vijana wa kitanzania wanaenda kusoma ,naomba niishuri serikali ione namna ya kuwapatia Mikopo vijana wanaoenda kusoma vyuo vikuu vya nje.” Amesema Kibetha 


Nakuongeza kuwa sisi kama UAR  tumekua tukiyashiriki Maonyesho haya kwa muda wa miaka zaidi ya 10 kutokana na ndoto au matarajio au mahitaji,hivyo imekua sehemu   ya vijana wengi yakuweza kujua kujua wapi waende wakasome.


Amesema kuwa changamoto kubwa iliyopo watu hawakujua nini cha kusoma hivyo walisoma vitu ambavyo leo havina soko nakwamba wamekuwa wakiwashauri  vijana yale waliyoyasoma kwa kuzingatia matakwa au sheria ya TCU kwamba yanakubalika katika nakwamba Tanzania  imefanikiwa.


Aidha ameendelea kusema kuwa Changamoto nyingine ni gharama ya kulipia ada kwenye vyuo vya nje  lakini UAR imefanikiwa kuleta  vyuo ambavyo vinatoa ufadhili  ( scholarship) ambapo ukienda kulipa ada ni sawasawa na vyuo vikuu  vya hapa Tanzania


“ Kikubwa ambacho tupo nacho sisi kwa awamu hii ya tatu ni kwamba nikuhakikisha wanafunzi wanaenda kusoma kwenye vyuo  ambavyo wanaweza kufanya kazi na  kupata kipato  ambacho wanaweza kujisaidia hata kwa ada, Nchi hizo ni Marekani,Ujerumani ,Poland pamoja na Hisapania.


Ameongeza kuwa mbali na hilo pia vijana wengi wana vipaji mbalimbali kulingana na uwezo wao, hivyo taasisi hiyo imepata nafasi katika nchi za Ujerumani na Hispania kuwapeleka vijana wenye vipaji ili kuendeleza vipaji vyao.


Amesema kuwa  UAR ni taasisi ya kwanza kutoka hapa Tanzania kwa kuweza kusaidia vijana kusoma na kupata ajira nje ya nchi, kitu ambacho kama Taasisi tunajivunia.


“Malaysia na China zilikua pamoja nasi katika miaka ya sabini lakini walifanya upendeleo kwa watu wao   kwenda kusoma nje ya nchi ili waweze kufanya kazi kutokana na  ile tknoloji waliyopata kutoka nje” amesema.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI