Teddy Kilanga_Arusha
Serikali imeanza mpango mkakati wa ujenzi wa kituo kikubwa cha mkutano kijulikanacho Mount Kilimanjaro Convesion kwa lengo la kuongeza bidhaa ya utalii ili kuwavutia wageni kutembelea vivutio vilivyopo mkoani Arusha na maeneo mengine nchini.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa serikali,Greyson Msigwa jijini Arusha alipotembelea eneo hilo linalotarajiwa kujengwa kituo hicho kikubwa ambapo alisema mkoa wa Arusha ni kitovu cha utalii nchini hivyo kuna haja ya kuongeza bidhaa za utalii ili kuwavutia wageni.
Msigwa alisema dhamira ya serikali ni kuhakikisha wanaongeza mapato yatokanayo na utalii ambapo lengo ni kufikia watalii milioni tano ifikapo mwaka 2025 ikiwa mwaka uliopitia walifikia watalii takribani milioni 1.4 kutokana na changamoto ya mlipuko wa ugonjwa wa covid 19.
"Hivyo tunapokwenda na safari hii tunahitaji miundaombinu kwa ajili ya kuwahifadhi watalii ili wanapofika kwa ajili ya mikutano wanaenda katika vivutio vya utalii mbalimbali hivyo naupongeza uongozi wa AICC kwa mpango huu,"alisema.
Alisema katika ujenzi wa miradi kuna haja haja kushirikisha sekta binafsi kuwekeza kwani ndio adhma ya serikali katika kufikia malengo yake hivyo anachowaomba watanzania kuendelea kushirikiana na serikali kwani mipango mbalimbali ya serikali imekuwa ikikosolewa na vikundi vya watu wachache.
"Wananchi tuache fitina katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya serikali kwani mafanikio yoyote yanataka uwekezajia ambao unashirikisha sekta binafsi,"alisema Msigwa na kuongeza kuwa lengo ni kuongeza mapato mengi yatakayosaidia kutoa huduma kwa serikali.
Alisema kituo cha kimataifa cha mkutano ni biashara katika jamii ikiwa bahati nzuri serikali imeunda chomba kijulikanacho kama AICC ndio wasimamizi wakubwa wa ujenzi wa mkutano huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi qa kituo cha kimataifa cha mikutano cha Arusha,Ephraim Barozi Mafuru alisema wanadhamira katika kuleta mapinduzi ya utalii wa mikutano hapa Afrika ambapo kwa kipindi cha miaka 45 tangu kuanzishwa kwa AICC imekuwa na kituo kimoja kilichopo jijini Arusha ambacho hadi sasa hakijaweza kikidhi haja ya sasa la soko la utalii wa mikutano.
Mfuru sliongeza kuwa mbali na uwepo wa kituo kingine cha Dar es Salaa cha JICC lakini pia Arusha kama kitovu cha utalii serikali imefanya maamuzi makubwa ya kuweza kuwekeza katika kituo kikubwa cha sasa cha mikutano.
"Eneo hilo la ujenzo wa kituo kikubwa cha mikutano ya kimataifa linaukubwa wa heka 21 ambapo ikijumuisha na maeneo mengine kinajumla ya eneo la eka 90 chenye urefu wa kilometa mbilo ikiwa lengo ni kubadilisha matumizi na kuwekeza kwenyw kituo kikubwa cha Mikutano ya kimataifa cha Mount kilimanjaro ambacho kitakuwa na ukumbi wa ukubwa wa kubeba wageni 3000 na eneo la maonyesho litakalochukua watu zaido ya 10000,"alisema Mafuru
Pia alisema katika kituo hicho kinachotarajiwa kijengwa kitakuwa na eneo la uwekezaji wa utalii ambapo wataanza na hoteli moja ya nyota tano ambapo mpango ni kiwekeza katika hoteli mbili zenye uwezo wa kuchukua watu 1000 katika eneo hilo.
0 Comments