Header Ads Widget

SERIKALI KUANZA KUTEKELEZA MAFUNZO YA AMALI

 



CHAUSIKU SAID_MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.


Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatarajia kufanya utekelezaji wa mpango wa Elimu ya Msingi na kutambua shule za msingi zisizo na Sekondari na kuongezewa ili kuwezesha kuwa na madarasa yatakayo toa mafunzo ya ujuzi na utendaji (MAFUNZO YA AMALI).


Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu, sayansi na teknolojia Profesa Adolf Mkenda katika ziara yake ya kukagua Miradi ya Maendeleo ya Elimu katika Wilaya ya Buchosa na Sengerema Mkoani Mwanza na kueleza kuwa shule zitakazoingia kwenye mpango huo zitakuwa na mafunzo Kwa vitendo.


Prof, Mkenda amesema kuwa Serikali inakusudia kuongeza madarasa ya kidato Cha kwanza hadi Cha nne katika shule za Msingi ambazo Kwa sasa hazina shule za sekondari.


" jukumu la kutambua shule hizo za  sekondari ni la Wizara Kwa kushirikiana na Tamisemi na tumeishaanza kazi hiyo ya kuzitambua shule hizo Nchi Nzima ambazo watajenga Sekondari na Msingi" Alisema Prof Mkenda.


Amesema kuwa mpango huo utaanzia baada ya sera na mtaala mpya wa Elimu kupitishwa utakaohusisha elimu ya Msingi kuoshia darasa la sita kabla ya mwanafunzi kufanya mtihani wa kuingia kidato Cha kwanza.


Prof, Mkenda ameeleza kuwa wanafunzi wataomaliza masomo ya kidogo Cha nne katika shule hizo watapatiwa vyeti vya kumaliza kidato Cha nne na mafunzo ya AMALI.



Katika hatua nyingine Prof Mkenda ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa tawi la chuo kikuu Cha Ardhi kampasi ya Mwanza kinachojengwa katika Kijiji Cha karumo Wilayani Sengerema .


Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradio huo Makamu mkuu wa chuo Cha Ardhi Profesa Evaristo Liwa ameeleza kuwa zaidi ya sh 17.8 bilioni zitatumika kujenga majengo matano ya kampasi hiyo.


Prof asema kuwa Asilimia 70 ya ghama hizo zitatumika kujenga majengo ya studio, utawala, ofisini za walimu, Makataba,bweni pamoja na zahanati huku Asilimia 30 iliyobaki itatumika kununuliwa thamani na uandaaji wa mitaala Kwa awamu ya kwanza ya mradi huo.


Mradi huo unatarajia kukamilika ndani ya miezi  15 ijayo, huku ikitegemea kuanza mwezi septemba mwaka huu.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI