Header Ads Widget

SERIKALI IMETENGA BIL.1 KWA AJILI YA UKARABATI WA MASOKO TEMEKE



Serikali imetenga kiasi cha shilingi Bil.1 kwaajili ya kufanya ukarabati wa masoko ndani ya Manispaa ya Temeke kwa lengo la kuboresha mazingira ya masoko wilayani humo.


Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mobhare Matinyi wakati akikagua Maendeleo ya Ujenzi wa soko jipya la kisasa  ameridhishwa na hali ya ujenzi wa soko jipya na la Kisasa la  Mbagala Kibonde Maji (Zakhiem) ambapo akimtaka mkandarasi wa soko hilo kulikabidhi kwa Manispaa ya Temeke ifikapo Agosti 15 ,2023.


Amesema ukarabati huo utafanyika sambamba na kufanya usafi katika masoko hivyo wamejipanga kuanzisha kampeni ya usafi ndani ya Manispaa ya Temeke itakayoanza hivi karibuni na kutekelezwa usiku na mchana.

 


Matinyi amesema Wafanyabishara wanaokaa pembezoni mwa barabara si wa Dar es Salaam pekee bali nchi nzima wanakua sawa na uchafu kutokana na kuzagaa hovyo barabarani.


Aidha amemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kiasi cha Bil.2.843 ambazo zimejenga soko hili jipa na la kisasa ndani ya Manispaa ya Temeke.


Matinyi alisema baada ya Mkandarasi kukabidhi soko hili kazi inayobaki ni kwa Mkurugenzi Elihuruma Mabelya wa Manispaa  ya Temeke,  Mstahiki  Meya wa Manispaa  ya Temeke Abdalah Mtinika  pamoja na Katibu  wa wafanya biashara katika  soko hili.


"Wakae pamoja na kupanga  namna Wafanyabishara watakavyo pangwa ndani ya soko huku kipaumbele kikiwa ni kwa wale wafanyabiashara ambao walikuwepo awali wakati wa lile soko duni la awali" amesema 



"Viongozi mtatakiwa  kusimamia mgawanyiko  wa vizimba vya biashara  kulingana na  ukubwa wa biashara zao na jumla ya  mamalishe 20 waliokuwepo awali watapewa kipaumbele ndani ya soko hilo" amesema Mheshimiwa Matinyi.


Amesema kuwa ujenzi wa soko hilo umechukua muda wa mwaka mmoja  kikamilifu  ambapo awali kulikua na soko duni ambapo hivi sasa  kuna  vizimba 160 hukumiundo mbinu ikiwa  ni rafiki  na kufikika kwa urahisi kwa ujumla.


Katika soko hili kutakua na ofisi za Manispaa ambao watasimamaia masuala ya msingi ndani ya soko pia kutakuwa na kitengo cha Tehama ambacho kitafunga mitambo maalumu ili kufuatilia nyendo zote za wafanyabiashara na utendaji wao kazi  ndani ya soko.



Hatahivyo Matinyi ametoa onyo kali kwa kuahidi kuwachukulia hatua kali Wafanyabishara ambao watafanya uhuni  endapo watapangishwa  kwa fedha ndogo ya serikali  halafu na wao wapangishe wafanyabiashara wengine.



Wakati huohuo Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Elihuruma Mabelya  amesema kuwa wamejipanga kuwaondoa wafanyabiashara ambao huzagaa hovyo pembezoni mwa barabara kwa kuwa wanakwenda kinyume na sheria huku akisisitiza kwa kusema kuwa Manispaa hiyo  wamejipanga  na wataanzisha kampeni ya kuwaondoa pamoja kuiweka Temeke safi kwa ujumla.










Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI