NA CHAUSIKU SAID_MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.
Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza limefanikiwa kumkamata Oswald Kaijage Binamungu mwenye umri (39) mhandisi wa umeme katika mgodi wa Geita Gold Mining (GGM) na Mkazi wa wa Buswelu Manispaa ya Ilemela aliyetoroka baada ya kusababisha ajali.
Ajali hiyo iliyohusisha gari lenye namba za usajili T.476DZL na Toyota Hilux Double Cabon iliyotokea siku ya jumamosi Julai 22.Mwaka huu majira ya asubuhi eneo la lumala katika barabara kiseke Wilayani Ilemela Mkoani na kusababisha vifo vya watu 6 na majeruhi 16.
Akizungumza na Waandishi wa habari Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani hapa Wilbroard Mutafungwa amesema kuwa watu hao waligongwa wakati wakifanya mazoezi ya mchaka mchaka ( Jogging Club).
Mtafungwa ameeleza kuwa majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospital ya Mkoa wa sekou Toure na hospital ya Kanda Bugando ambapo hospital ya sekou Toure wamebaki majeruhi 4 na Bugando 5.
Aidha katika hatua nyingine Kamanda Mutafungwa amevikumbusha vikundi vya mchaka mchaka (Jogging) kusajiri vikundi vyao kwenye ofisi za utamaduni katika ngazi za Wilaya,Manispaa na Jiji ambapo watapewa miongozo au maelekezo ya namana bora ya kufanya mazoezi kwa kuzingatia hali ya usalama wao na watu wengine.
"Tunakumbusha vikundi hivyo kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi katika Wilaya husika endapo watahitaji kutumia barabara wakati wa mazoezi yao ili askari wa usalama barabarani waweze kusimamia usalama wao na watumiaji wengine wa barabara ambao kwa wakati huo watakua wanatumia barabara hizo ili kuepusha ajali.
0 Comments