Na Fadhili Abdallah,Kigoma
MAMLAKA ya mapato (TRA) mkoa Kigoma imesema kuwa kuanza kutekeleza majuku yake kwa dawati la uwezeshaji la mamlaka hiyo kutawezesha kutekelezwa kikamilifu kwa changamoto za wafanyabiashara zinazojitokeza ili kupatiwa ufumbuzi wa haraka.
Meneja wa TRA mkoa Kigoma, Beatus Nchota alisema hayo mjini Kigoma wakati wa uzinduzi wa dawati hilo ambalo alibainisha kuwa limeanzishwa kwa malekezo ya Raisi Samia Suluhu Hassan baada ya kuona kuwa uwezeshaji wa wafanyabiashara una manufaa makubwa katika kukuza uchumi wa nchi hivyo dawati hilo limeanzishwwa kukabiliana na changamoto zinazojitokeza.
Meneja wa TRA mkoa Kigoma Beatus Nchema
Nchota alisema kuwa dawati hilo litawaleta pamoja wafanyabishara katika suala la ukusanyaji kodi lakini pia kuhakikisha wanawasaidia kuwawekea mazingira mazuri ikiwemo kukutana na taasisi nyingine ili shughuli za biashara zisikwame kulingana na changamoto zinazojitokeza na wafanyabiashara wadogo waweze kukua.
Katibu wa Chama cha Wafanyabishara, wenye viwanda na kilimo (TCCIA) mkoa Kigoma, Prosper Guga
Sehemu ya wafanyabiashara wa mkoa Kigoma wakifuatilia uzinduzi wa dawala la uwezeshaji la TRA mkoa Kigoma
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Wafanyabishara, wenye viwanda na kilimo (TCCIA) mkoa Kigoma, Prosper Guga alisema kuwa kumekuwa na changamoto kubwa kwa wafanyabiashara wanaovuka mpaka na wamefanya kazi kubwa kukabiliana na changamoto hiyo hivyo wanaamini dawati hilo litawaleta pamoja katika kuzishughulikia changamoto za wafanyabiashara zinazojitokeza na kuzipatia ufumbuzi wa haraka ili kuwezesha biashara kukua na kukuza uchumi wa nchii.
Akizindua dawati hilo Mkuu wa mkoa Kigoma,Balozi Simon Sirro ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa wilaya Kigoma, Dk.Rashid Chuachua alisema kuwa dawati hilo ni maelekezo ya Raisi Samia hivyo wao kama wasaidizi wa Rais Watasimamia kwa karibu kuona dawati hilo linatekeleza majukumu yake kikamilifu bila urasimu na kuchukua hatua kwa watendaji ambao wataenda tofauti na malengo ya dawati.
0 Comments