NA HADIJA OMARY,LINDI
Jeshi la polisi mkoani Lindi limethibitisha kuwa kijana simoni manyoli (30) mkazi wa mtaa wa msonobalini chini kata ya msinjahili Manispaa ya Lindi Mkoani humo aliejikata sehemu yake ya siri (uume) yeye mwenyewe ni mgonjwa wa akili
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa Habari na kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi ACP Pilli Omary Mande alisema tukio hilo lilitokea jana majira ya saa tatu kamili asubuhi ambapo kijana huyo alijikata kwa kutumia kitu chenye ncha kali sehemu za siri (uume na kuundoa akabisa) akiwa chumbani kwake kwenye nyumba aliyopanga.
ACP pilli Mande alisema Mtu huyo mara baada ya kujikata alitoka katika chumba chake akiwa uchi na damu zikimtoka nyingi huku akikimbilia baharini ambapo alipofika alianza kuosha jeraha hilo kwa maji ya bahari.Hata hivyo raia wema walitoa taarifa kituo cha Polisi na hatimaye Polisi walifika na kumchukuwa kisha walimpeleka kupatiwa matibabu katika hospitali ya Sokoine Lindi.
Alisema Jeshi la Polisi liliweza kubaini ndani ya chumba chake ambacho anaishi peke yake, chupa ndogo ya kilevi aina ya Smart Gin ambayo ilikuwa nusu pamoja na dawa ambazo madaktari walisema zilikuwa ni za kutibu magonjwa ya zinaa.
Hata hiyo kwa mujibu wa kamanda wa polisi alisema meneja huyo amebainisha kuwa Muhanga anahistoria ya kuugua ugonjwa wa afya ya akili kwa muda wa mwaka mmoja kipindi cha nyuma ,na alilazwa katika wodi ya watu wenye matatizo hayo katika hospitali ya Bugando mkoani Mwanza.Ameongeza kuwa amekuwa na tabia ya kuvua nguo hali hiyo inapomrudia na hasa anapokuwa na msongo wa mawazo.Muhanga amelezwa katika hospital ya Sokoine akiendelea kupatiwa matibabu.
0 Comments