Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe.Antony Mtaka
Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NjombeUshiriki duni wa wanaume katika masuala ya lishe,Mapokeo madogo ya elimu ya lishe pamoja na kuchelewa kwa fedha za utekelezaji wa mkataba wa lishe mkoani Njombe ni miongoni mwa sababu zinazotajwa kukwamisha jitihada za kukabiliana na utapiamlo na udumavu kwa watoto.
Katika kikao Cha tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe mkoani Njombe taarifa za hali ya lishe kwenye Halmashauri sita za mkoa zimeonyesha kuwapo kwa changamoto mbalimbali ikiwemo ushiriki hafifu kwa wanaume pamoja na bajeti ndogo Jambo linalokwamisha jitihada za kukabiliana na suala hilo.
Afisa lishe mkoa wa Njombe Bertha Nyigu anakiri kuwa fedha zimekuwa kikwazo katika utekelezaji wa mkataba wa lishe Jambo ambalo linapaswa kufanyiwa kazi.
Baadhi ya wakuu wa Wilaya akiwemo Claudia Kitta toka Wanging'ombe na Victoria Mwanziva mkuu wa wilaya ya Ludewa wamesema wameendelea kuongeza ubunifu katika kukabiliana na Changamoto ya udumavu.
Kwa Upande wake mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesema uwepo wa Viongozi Wengi wanawake katika mkoa wa Njombe kusaidie kupunguza udumavu kwa watoto.
Wakazi wa Njombe wanasema majuku ya kiuchumi yanawafanya kukosa muda wa kuwalea vyema watoto huku wakiwataka wataalamu kutokata tamaa ya kuwaelimisha.
Mkoa wa Njombe hivi sasa unashika nafasi ya pili Kitaifa kwa Udumavu kwa kuwa na asilimia 50.4 huku mkoa wa Iringa ukiwa Kinara kwa asilimia 56.9.
0 Comments