Header Ads Widget

RAIS SAMIA KUFUNGUA MKUTANO WA SITA WA DUNIA WA MASUALA YA USAWA WA KIJINSIA NA HAKI ZA WANAWAKE NCHINI RWANDA

 



 Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kufungua mkutano wa sita wa kuongeza uhamasishaji katika masuala ya usawa wa kijinsia haki na ustawi wa wasichana na wanawake katika nyanja zote Women Deliver Conference ambao kwa mara ya kwanza unafanyika barani Afrika nchini Rwanda na kuhusisha wanawake kutoka mataifa mbalimbali duniani.


Hayo yamesema wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii , jinsia, wanawake na makundi maalum Dr. Dorothy Gwajima wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu mkutano huo ambao mwaka huu utafanyika katika jiji la Kigali, Rwanda kuanzia tarehe 17 hadi 20 Julai mwaka huu.


Amesema Waziri huyo wa Maendeleo ya Jamii , jinsia, wanawake na makundi maalum pia ndiye atamwakirisha Mheshimiwa Rais katika mkutano huo nchini Rwanda.


Amesema Mkutano huo utaleta pamoja wanawake katika ngazi ya jamii, asasi za kiraia, wanaharakati vijana, serikali na wadau wa maendeleo kubadilishana uzoefu na kujadili hatua muhimu zinazohitajika ili kuendeleza haki za ardhi za wanawake, mazingira, masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na masuala ya afya. 


“Watoa mada watajadili jinsi haki na milki salama za ardhi za wanawake zilivyo na nyenzo ya kuendeleza usawa wa kijinsia na maendeleo endelevu kwa kutatua migogoro, kukabiliana na majanga ya mara kwa mara, na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi , usalama wa chakula, na umaskini"

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI