Header Ads Widget

NAY WA MITEGO AITWA BASATA, ASHINDWA KUHUDHURIA

 


Na Simon Joshua-Matukio Daima, Dar es salaam.

Msanii wa mziki wa kizazi kipya, Emmanuel Elibariki maarufu kwa jina la Nay wa Mitego kupitia kurasa zake za kijamii zake za kujamii amefunguka kuitwa na Baraza la Sanaa la taifa (BASATA) kwa ajili ya mahojiano juu ya wimbo wake mpya kwa jina la Amkeni alioutoa hivi karibuni na kusema kuwa ameshindwa kufika katika mahojiano yako kutokana na kuwepo safarini.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nay wa Mitego ameandika ”Wameniambia nahitajika Kwenye kikao Asubuhi Ya leo saa nne, kujadili wimbo wangu wa Amkeni, Barua imenifikia leo Asubuhi na walikuwa wanataka niende Asubuhi Ya leo leo Sasa huoni kama kitu kidogo hakiko sawa na Kwa bahati mbaya mimi nimesafiri, Mwanasheria amewasiliana nao Nadhani kama kutakua na ratiba mpya ya kikao nitahudhuria,  nahisi kurudi Jumatatu, wimbo wangu hauna ukakasi, ukiona mpaka wimbo nautoa umeshapitiwa na watu wengi ushaeditiwa sana mpaka unatoka”

"Sema tu Kwa Sababu watu hawapendi ukweli, ni wimbo ambao nimezungumza Maisha ya kila mtu, Ukumbuki utaratibu wa kupeleka wimbo usikilizwe kwanza ushatolewa, ilikuwa sio lazima, tutaangalia siku hiyo itakavyokua, mimi nafanya kwaajili ya Jamii yangu” Aliongeza Nay.

Nay wa Mitego amekuwa akifahamika kwa kuimba nyimbo zenye ujumbe mzito na amekuwa akitumia sauti yake kutoa maoni yake kuhusu masuala ya jamii. Wimbo huu mpya umezua hisia mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii na unatarajiwa kuwa moja ya nyimbo zinazosikilizwa sana nchini Tanzania.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI