Header Ads Widget

NDEGE YA JWTZ YAPATA AJALI BAADA YA KULAZIMIKA KUTUA KWA DHARULA UWANJA WA NDEGE MANISPAA YA BUKOBA.

 









Na Theophilida Felician Kagera.


Ndege yenye namba za usajili 9127 Mali ya Jeshi la wananchi Tanzania JWTZ imepata ajali na kuanguka maeneo ya uwanja wa ndege  Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.



Akizungumzia  juu ya kutokea kwa ajali ya ndege hiyo kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Kagera ACP BLASIUS Z, CHATANDA amesema kuwa tukio hilo limetokea  hii Leo tarehe 20 Julay mwaka 2023 mnamo majira ya saa tatu na nusu 3:30 asubuhi.



Kamanda Chatanda amefafanua kuwa ndege hiyo ilikuwa katika mafunzo yanayoendelea ambapo ndani yake walikuwemo marubani wawili ambao ni Meja Renadi Revokatus  Mkundwa Muha mwenye umri wa miaka (45) pamoja naye Luteni Alex Venance Moshi Mchaga umri miaka 30.



Amesema kuwa  watu hao wawili   wamepelekwa  Hosptalini na kufanyiwa uchunguzi kiafya  hivyo wamebainika kuwa salama na kuruhusiwa.



Hata hivyo ameongeza kuwa chanzo cha ajali ya ndege hiyo hakikufahamika mara moja na uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha ajari hiyo.



Mkuu wa wilaya Bukoba Erasto Sima amewashukuru  jeshi la zima Moto na uokoaji pamoja na wadau wengine waliojitokeza na kuwahi kufika eneo la tukio mapema hatimaye  kusaidia kuwaokoa marubani hao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI