Header Ads Widget

KATIBU MKUU YAKUBU AELEZA MIPANGO YA SERIKALI KUJENGA MIUNDOMBINU YA MICHEZO NCHINI

Na Eleuteri Mangi-Matukio Daima, Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amesema Serikali imepanga kujenga viwanja viwili vya michezo nchini katika mkoa wa Arusha na Dodoma ili vitumike katika michuano mbalimbali barani Afrika na Duniani vyenye uwezo wa kuchukua watazamaji 30,000 kila mmoja.



Pichani: Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu akieleza mpango wa Serikali katika kuboresha Uwanja wa Benjamin Mkapa alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa China Julai 24, jijini Dar es Salaam

Bw. Yakubu amesema hayo Julai 24, jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa China uliomtembelea ofisi ndogo jijini humo ambapo amesisitiza kuwa kuna fursa ya ushirikiano katika kujenga miundombinu ya michezo katika maeneo mbalimbali nchini.

Aidha, Serikali imejipanga kuboresha na kukarabati viwanja saba vya Uhuru, Uwanja wa Benjamin Mkapa vya Dar es Salaam, Uwanja wa Sheikh Abeid Arusha, Uwanja wa Sokoine Mbeya, Uwanja wa Jamhuri Dodoma, Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza na Mkwakwani Tanga.


Pichani: Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya CREC Bw. He Yeting kutoka nchini China akifafanua jambo wakati wa ziara yao walipotembelea Uwanja wa Benjamin Mkapa alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa China Julai 24, jijini Dar es Salaam

Amesema pia Serikali inajenga pia Viwanja vya wananchi kupumzikia katika jiji la Dar es Salaam na Dodoma pamoja na Arena mbili katika mikoa hiyo.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya CREC Bw. He Yeting kutoka nchini China amesema wataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika eneo la kuboresha miundombinu ya michezo hapa nchini kuilingana na mahitaji ya wakati huu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI