Na WILLIUM PAUL, MOSHI.
Mgombea Ubunga wa Jimbo la Moshi Mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Ibrahim Shayo ameahidi kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi na kijamii endapo atachaguliwa, huku akibainisha vipaumbele tisa muhimu atakavyovishughulikia kwa haraka.
Shayo alitoa kauli hiyo jana wakati akizindua kampeni zake katika viwanja vya Mandela ambapo alisema ndoto yake ya zaidi ya miaka 30 sasa imefikia hatua ya utekelezaji, akisisitiza kuwa yuko tayari kuwatumikia wananchi wa Moshi kwa uaminifu na uadilifu.
Huku akitaja baadhi ya vipao mbele vyake atakapopewa ridhaa ni uwazi mdogo kati ya Mbunge na wananchi.
"Nitahakikisha nakuwa karibu na watu wangu. Sitakuwa Mbunge wa kusafiri tu, nitakuwa hapa Moshi, nikisikiliza na kushughulikia changamoto zenu moja kwa moja," alisema.
Katika ahadi nyingine, Shayo alisema atahakikisha stendi ya Ngangamfumuni inaboreshwa na kufikia viwango vinavyostahili.
"Stendi hii itakuwa historia mpya ya usafiri Moshi. Tutaiweka kwenye ramani ya kisasa," alieleza
0 Comments