Header Ads Widget

JAMII, WADAU WATAKIWA KUWEKA NGUVU YA PAMOJA KUKABILIANA NA TATIZO LA TABIANCHI

 



Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


MKURUNGENZI wa huduma za Sheria  Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Dastan Shimbo Amesema ili kukabiliana na tatizo la mabadiliko ya Tabianchi nguvu ya pamoja kwa wadau na jamii kwa ujumla .


Hayo yameelezwa jijini Dodoma kwenye mkutano wa ufungaji wa mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi,Dodoma na Pwani.


Amesema ili kuwa na Tanzania ya kijani kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho katika kutunza Mazingira kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi dhamira ya dhati inaitajika kwa wadau na hata jamii kwa ujumla


Shimbo amesema kuwa mradi huo wa mabadiliko ya Tabianchi umeifunza serikali umuhimu wa kushirikiana katika kutatua changamoto mbalimbali za kijamii hapa nchini.


Kutokana na hilo amewaomba wadau hasa mashirika ya kibiashara kujitokeza kuunga na na serikali katika kushughulikia changamoto mbalimbali na kuliletea maendeleo taifa na wananchi kwa ujumla.


"Tumeshuhudia taasisi za serikali zikiungana na taasisi za kimataifa na mashirika ya kibiashara na kuweza kufanya kazi kwa ufabisi mkubwa,"amesema Shimbo.


Amesema tunakwenda kuufunga mradi wa mabadiliko ya Tabianchi Kuna haha ya kusherehekea mafanikio kutafakari na kujadili changamoto zilizojitokeza na yale yaliyoanzishwa hayapotei wala kuharibika


"Ni matamanio yangu kuona miti yote itakayokabidhiwa inakuwa na kuleta mabadiliko tuyatakayo ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani,"amesema Shimbo.


Aidha ametaka wanafunzi wote waliosaidiwa na kuelimishwa katika upandaji miti waendeleze elimu hiyo si mashuleni na vyuoni kwao tu bali hata kwenye familia zao na jamii zinazowazunguka.


"Tunataka moto huu ufike huko mitaani ili kila mwananchi awe mdau katika uhifadhi wa mazingira,vikundi vya vijana na kinamama vilivyowezeshwa kwa namna mbalimbali tunategemea muwe mabalozi wazuri kwenye ulinzi na uhifadhi wa misitu yetu lakini pia tuone maisha yakiwa bora zaidi,"amesema.


Pamoja na hayo Shimbo amewaagiza Watendaji wa Serikali wa jiji la Dodoma,Ofisi ya Makamu wa Rais na taasisi zilizonufaika na mradi huo kuhakikisha miradi hiyo inaendelezwa na kuboreshwa kwa kuanzia walipoishia WWF.


"Wamesema kuwa wanapofunga mradi huu sasa wametukabidhi rasmi pia miradi hii iwe imekufa na kupoteza rasilimali zote zilizowekezwa hapa,tujitahidi najua tutaweza kuwa na changamoto ya uwezeshaji lakini tuhakikishe tunatafuta rasilimali zaidi na hata wadau wengine ili hata Vodacom Tanzania na WWF wakija miaka michache ijayo wakute maeneo yote yamekuwa bora zaidi,


"Pale Medeli tunatamani kuona maono yao ya kupafanya kuwa msitu wa jiji naeneo la kupumzikia yakikamilika na ofisi yangu itakuwa tayari kushirikiana  na wadau wengine kuhakikisha hili linakamilika,"amesema.



Awali Mratibu wa Mradi wa Shirika la WWF,Savinus Kessy alisema kuwa lengo la mradi huo  ilikuwa ni kuelimisha jamii kupitia vyombo vya Habari na kuelimisha watanzania kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi huku akitaja  mradi huo ulianza rasmi Mwaka 2019 kupitia Mpango wa kuhamasisha upandaji miti.


Naye Iman Mahajile Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Mazengo amesema kuwa  kupitia mradi wa WWF wamepata manufaa mbalimbali ikiwemo kivuli wanafunzi kupumzika.


"Natamani kuona tukiendelea kupanda na kuitunza miti kwajili ya manufaa ya afya zetu,"amesema mwalimu Mahajile.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI