Header Ads Widget

MNEC VIJANA TAIFA AWATAKA VIJANA KUZINGATIA NIDHAMU KAZINI

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Vijana nchini wametakiwa kuzingatia nidhamu na weledi pindi wanapopata fursa ili waweze kutimiza ndoto zao na kuwasaidia wengine.



Akifunga mafunzo  ya Labour Based Teknology yaliyoandaliwa na umoja wa vijana UVCCM Mkoa wa Njombe yakilenga kuwafundisha vijana kazi za matengenezo ya miundombinu ya barabara  Mjumbe wa baraza kuu  CCM Taifa anayewakilisha vijana Mhe.Muhsin Hussi toka Zanzibar amesema nidhamu ndio nguzo pekee itakayowakomboa vijana katika maisha na hata pale watakapobahatika kupata kazi kwenye maeneo mbalimbali.


Aidha Mwenyekiti wa umoja wa vijana Uvccm mkoa wa Njombe Mhe.Samuel Mgaya amesema kutokana na changamoto kubwa ya ajira kwa vijana wengi nchini alilazimika kubisha hodi Tarura na Tanroads kuona uwezekano wa kuwasaidia vijana na ndipo akapewa maelekezo ya kuwataka kwanza wapate mafunzo hayo.


Naye Meneja wa Wakala wa barabara mijini na vijijini Tarura wilaya ya Njombe Mhandisi Costantine Ibengwe kwa niaba ya Mratibu wa Tarura mkoa wa Njombe amesema mafunzo hayo yatakuwa na tija kubwa kwa vijana hao katika siku za usoni kwani wamejiwekea hazina kubwa katika kutoa ajira kwa wengine.


Katibu wa umoja wa vijana UVCCM mkoa wa Njombe Ally Kachinga amesema kutokana na gharama kubwa za mafunzo hayo Chuoni walilazimika kuomba yatolewa mkoani Njombe kwa kila mmoja kuchangia shilingi 105000 pamoja na chakula.

Kwa upande wao baadhi ya vijana waliopatiwa mafunzo hayo akiwemo Salome Kasisi,Marry Songa na Edson Ngimbudzi  wanaiomba serikali kuwatizama kwa jicho la pekee pindi kazi ndogondogo za ujenzi zinapopatikana ili wajikwamue kimaisha. 


Zaidi ya vijana 140 toka mikoa 8 ya Singida,Katavi,Mbeya,Songwe,Rukwa ,Lindi,Mtwara na Njombe wameshiriki mafunzo ya Labour Based Teknology kwa muda takribani  mwezi mmoja na hatimaye kkutunukiwa vyeti baada ya  kuhitimu.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI