Header Ads Widget

MNEC ATOA MAELEKEZO KWA VIONGOZI WA HALMAAHAURI,CCM WANAOGOMBANA

 


Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa ya CCM mkoa Kigoma Abdulkadri Mushi (katikati) akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ikiwa ni ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM

Na Fadhili Abdallah,Matukio Daima App Kigoma

MJUMBE wa halmashauri kuu ya Taifa ya CCM mkoa Kigoma Abdulkadir Mushi amezitaka kamati za siasa za wilaya za CCM mkoani Kigoma kutumia vikao,kanuni na miongozi kushughulikia migogoro na mahusiano mabaya ya viongozi wake na viongozi wa serikali kwani imekuwa chanzo kikubwa cha kukwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi.

Mjumbe huyo wa NEC alisema kuwa ugomvi wa viongozi ndani ya chama, ugomvi wa viongozi wa chama na watendaji wa halmashauri na ugomvi baina ya viongozi wa chama na viongozi wa serikali umekuwa na athari mbaya katika upangaji na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo inakusudiwa kwenda kwa wananchi.


Mushi alishuhudia hayo  wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya mkoa Kigoma kutembelea miradi ikiwa ni sehemu ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM na kushuhudia kukwama kwa ujenzi wa jengo la utawala la Halmashauri ya wilaya Kigoma kwa miezi 18.

Taarifa za kukwama kwa mradi huo zinabainishwa kwenye taarifa mbalimbai wakati wa ziara hiyo na hasa  kuwepo kwa  mahusiano mabaya ya viongozi ndani ya halmashauri hiyo sambamba na  mahusiano mabaya ya viongozi wa halmashauri hiyo na CCM na kuzua makundi ambayo yanapingana kwa kila jambo lilalopangwa.

Mjumbe huyo wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM alisema kuwa anajua kuwepo kwa mahusiano duni baina ya Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kigoma Vijijini  dhidi ya Katibu wa wilaya hiyo,  mahusiano Duni Baina ya Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazinii dhidi ya Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, mahusiano mabaya baina ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo dhidi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Kigoma.

“hatuwezi kukubaliana na suala hili lazima hatua zichukuliwa, mwenyekiti wa CCM wilaya tumia vikao, kanuni na miongozo kushughulikia jambo hilo kwani linatukwamisha,lete mashitaka kwenye kamati ya maadili ili vikao vifanye kazi yake na kulishughulikia jambo hilo” Alisema Mjumbe huyo wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.

Mhandisi huyo wa ujenzi alisema kuwa mgogoro huo kwa kiasi kikubwa unatokana na masuala ya kisiasa na

 kuzua makundi ambayo kila moja lilikuwa linataka eneo ambalo wanaona kisiasa litafaa kujengwa kwa mradi huo na ndiyo sababu mradi ukachelewa kuanza licha ya kuwepo kwa fedha kiasi cha shilingi Bilioni mbili zilizotolewa kwa awamu mbili.


Mhandisi wa ujenzi wa halmashauri ya wilaya Kigoma Tecla Lyubha akitoa taarifa ya hali ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa jengo la utawala la halmaahauri ya wilaya Kigoma

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI