ABIRIA 57 waliokuwa wakisafiri na basi la kampuni ya New Force kutoka Mbeya Kupeleka Dar es salaam wamenusurika kifo baada ya basi Hilo kupinduka Katika Mlima Kitonga mkoani Iringa .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Allan Bukumbi amethibitisha kutokea Kwa ajali hiyo na kuwa basi hilo lenye usajili namba
T448DDT Zong Tong Mali ya Kampuni ya NewForce Enterprises Ltd kuwa
abiria wake wote 57 wako salama na hakuna majeruhi yeyote katika ajali iliyotokea eneo la Mlima Kitonga wilaya ya Kilolo barabara kuu ya Iringa Morogoro baada ya basi la Kampuni ya New Force kupinduka na kulalia upande mmoja Kando ya barabara.
Ajali hiyo ilitokea saa 3:30 asubuhi leo Julai 2, 2023 ambapo basi hilo aina ya Yutong lilikuwa limebeba abiria 57 likitokea mkoani Iringa kuelekea jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Matukio Daima Media Kwa Njia ya simu Kamanda Bukumbi amesema basi hilo lilipinduka na kuegama pembezoni mwa barabara wakati dereva akiyapita mabasi mengine yaliyokuwa yanateremka katika mlima huo yakiwa kwenye foleni.
0 Comments