Header Ads Widget

MBUNGE ZUWENA ATAKA WANANCHI KUWAPUUZA WATU WENYE NIA HOVU NA TAIFA.

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI.

WANANCHI wametakiwa kuwapuuza baadhi ya watu wenye nia ovu kwa Serikali ambapo wamekuwa wakieneza taarifa za uongo kuhusiana na kuuzwa kwa bandari wakati sio kweli.


Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Viti maalum kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Zuwena Bushiri wakati wa Mkutano wa hadhara wa wakinamama wa kata ya Karanga manispaa ya Moshi.



Alisema kuwa, hakuna mkataba wowote wa kuuzwa kwa bandari ya Dar es salaam ambapo lengo la Serikali ni jema la kumtafuta mwekezaji ambapo watakaonufaika na uwekezaji huo ni wananchi Watanzania.


"Bandari hii ni mali ya Watanzania na hakuna mkataba wa mauziano wapo watu wachache wasiopenda kuona nchi yetu ikiendelea wamekuwa wakieneza taarifa za uongo kuwa bandari hiyo imeuzwa sio kweli wapuuzeni" alisema Mbunge Zuena.



Aidha Mbunge huyo aliwataka wananchi kujitokeza katika mikutano ya hadhara ya viongozi wa Serikali pamoja na chama cha Mapinduzi ili kusikiliza ukweli kuhusu bandari na kuelewa kuliko kuwasikiliza watu wenye nia hovu na Taifa.


Katika hatua nyingine Mbunge huyo aliwataka wakinamama kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa mwakani pamoja na uchaguzi mkuu 2025 ili kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hasani.



"Tunaelekea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa mwakani na ule uchaguzi mkuu 2025 wakinamama wenzangu tujitokezeni kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi lakini pia tumpe kura nyingi na za kishindo Rais Dkt Samia Suluhu Hasani" alisema Zuena.


Aidha Mbunge huyo aliwataka wakinamama kuzisemea kazi zilizofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hasani katika sekta mbalimbali ili wananchi watambue juhudi ambazo amekuwa akizifanya.

Mwisho...

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI