Header Ads Widget

"KINACHOTOFAUTISHA NCHI NA NCHI NI ELIMU NA SIO UTAJIRI" PROF. MKENDA

 Na Chausiku Said - Mwanza

Waziri wa Elimu  Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda ameeleza kuwa Nchi nyingi zinatofautiana kiuchumi Kwa sababu ya uwekezaji katika elimu sayansi na Teknolojia na sio utajili.

Hayo ameyabainisha wakati akifungua mafunzo ya Maafisa elimu kata 636 kati ya 1175 ambao wanapatiwa mafunzo ya uendeshaji na usimamizi wa mafunzo endelevu Kwa walimu kazini (MEWAKA) katika Chuo Cha Ualimu Butimba Mkoani Mwanza kutoka Mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Arusha, Singida, Manyara, Tabora na Dodoma.

Prof Mkenda ameeleza kuwa lengo la mafunzo Hayo ni kuimarisha matokeo ya ufundishaji na ujifunzaji katika ngazi ya shule za Msingi kupitia MEWAKA.

Amefafanua kuwa mtu anapaswa kutazama Maendeleo na sio uchumi ambapo Kila Nchi imetengeneza kitu kinachounda  vitu vitatu ambavyo ni pamoja na kipato, elimu na Afya.

Ameeleza kuwa kutokana na watu wengi kupima utoafauti wa Nchi na Nchi Kwa kuangalia utajili na chanzo chake kikiwa ni kipato.

"Imekuwa ni kawaida watu kusema Tanzania na Korea mwaka 61 hatukutofautiana sana na Nchi hiyo yenye utajili" Alisema Prof, Mkenda.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Elimu Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi wa mafunzo Kwa Walimu Tanzania Nicholas Magige ameeleza kuwa Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia (WYEST) iliandaa kiunzi Cha mafunzo endelevu ya walimu kazini mwaka 2020.

Magige ameeleza kuwa kiunzi hicho kilitiliwa mkazo kufanyika Kwa MEWAKA katika Ngazi ya shule, vituo vya walimu na vyuo ili kuongeza ujuzi na ufanisi katika kutafsiri na kuteketeza mtaala unaozingatia ujuzi na umahiri.

" Mafunzo haya yanalenga kumjengea mwalimu umahili katika kutumia stadi za Karne ya 21 ili kuboresha ujifunzaji wa wanafunzi wa Elimu ya awali na Msingi" Alisema Magige.

Maafisa Elimu kata wanajukumu la kuendesha na kisimamia MEWAKA katika Ngazi ya shule na vituo vya walimu.

" Kwa kuzingatia miongozo iliyopita sasa maafisa elimu kata ndio waratibu wa vituo vya walimu Kwa kuzingatia umuhimu wao" Alisema Magige.

Baada ya mafunzo Hayo kukamilika watakuwa wamefikiwa zaidi ya walimu 45,979 na viongozi wa Elimu 3412 katika mamlaka za serikali za mtaa pamoja na maafisa elimu kata 2,730 kutoka Halmashauri 184 watakuwa wamejengewa uwezo wa kuendesha na kisimamia MEWAKA katika shule na vituo vya elimu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI