Header Ads Widget

JUMUIYA YA WAZAZI YATAKIWA KUJIPANGA NA CHAGUZI 2024/2025.

 


Na Mbaruku Yusuph, Matukio Daima APP Tanga. 


JUMUIYA ya Wazazi Mkoani Tanga wametakiwa kutambua agenda waliyokuwa nayo mbele yao ni ya kuweka mikakati ya ushindi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 na uchaguzi Mkuu mwaka 2025.


Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Tanga Rajabu Abdurahman alipofungua Mkutano wa Jumuiya ya Wazazi Mkoani Tanga uliofanyika Wilayani Pangani Mkoani hapa.


Mwenyekiti huyo alisema viongozi wa Jumuiya zote wanapaswa kutambua kuwa chama kinakwenda kukabiliana na chaguzi hizo ambapo mwaka 2024 malengo ya chama hicho ni kushinda nafasi zote za Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Vijiji, na Vitongoji sambamba na uchaguzi Mkuu mwaka 2025 kwa nafasi za Madiwani, Wabunge na Rais. 


Alisema chama kinachangamoto pamoja na Jumuiya zake na kiongozi mzuri baada ya kuchaguliwa na kupewa dhamana kwa nafasi yake anaowajibu wa kukabiliana na changamoto zilizopo badala ya kuzikimbia.


Aidha alisema Viongozi wa Jumuiya hiyo waanze kujitathmini na watambue kuwa wanao wajibu wa kuboresha miradi na kuibua mipya ili kutengeneza kipato kikubwa kitakachoweza kukabiliana na changamoto zilizopo. 


Alisema ni wakati wa kuibadilisha Jumuiya hiyo kiutendaji na isifanye kazi kimazoea na viongozi wanapaswa kutambua kulegea kwa jumuiya hiyo sambamba na zile za Vijana na Wanawake kunaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kulegea kwa chama ambapo kinaweza kusababisha malengo yasitimie.


"Labda niweke wazi tu lazima sisi viongozituwe wa kwanza kuanza kujitathmini namna tunavyo tekekeza majukumu yetu na mjue kwamba mnafanya vikao viwili kwa mwaka hakikisheni mnaweka mipango kazi badala ya kukutana tu"Alisema Abdurahman. 


Awali akizungumza katika Mkutano huo Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Hassan Mbezi alisema baada ya kumalizika kwa Uchaguzi viongozi wa Jumuiya hiyo walianza kufanya ziara rasmi kwa ajili ya kutembelea rasilimali za Jumuiya hiyo.


Mbezi alisema katika ziara hiyo walitembelea shule ya Mombo,Lushoto,kwasanga,Boza na ile ya kidereko zinazomilikiwa na Jumuiya hiyo kwa lengo la kuangalia changamoto zinazozikabili shule hizo na kuzitafutia njia sahihi ya ufumbuzi.


"Mwenyekiti wetu,tumefanya vikao mbalimbali baada ya uchaguzi na tumekubaliana ndani ya miaka mitano tutahakikisha tunafanya vikao katika Wilaya tofauti ili tubadilishane uzoefu na leo tumeanzia na Wilaya ya Pangani "Alisema Mbezi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI