Header Ads Widget

TUNACHOTAKA NI KUBORESHA BANDARI YETU - ULEGA

 


Waziri wa Uvuvi na Mifugo ambaye pia mbunge wa jimbo la mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega amesema tunachotaka ni kuboresha bandari yetu na sio kuiuza bandari yetu kama wanavyosema wapotoshaji wanaopinga uwekezaji wa bandari.


Amesema hayo katika kijiji cha Magodani Kata ya Vikindu wilayani Mkuranga wakati alipokuwa akiongea na wananchi baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Zahanati ya Magodani ambayo itawapunguzia umbali wa kufuata huduma za afya zaidi ya kilomita 8 kutoka Magodani hadi Vikindu mjini.Ulega amesema kuhusu uwekezaji wa bandari ya Dar es salaam wkuna watu wametafuta upenyo wa maneno ya uchonganishi wakisema bandari imeuzwa.


“Kauziwa nani kwa bei gani na kiasi gani, yanayosemwa ni uongo mtupu, hofu yao ni kwamba tunakwenda kupiga hatua za maendeleo, jambo jema na zuri siku zote litapata mtikisiko mkubwa” amesema.



Amesema kazi yetu sisi Watanzania ni kumuunga mkono kinara wetu iwe jua iwe mvua tumuunge mkono Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Amesema vipengele vyote vya mkataba kuanzia kipengele cha kwanza mpaka cha Mwisho hakuna mahali palipozungumza kwamba bandari yetu inauzwa.


“Hakipo kipengele hicho, watu wametengeneza propaganda wakawahi sokoni wakawahi kwa wananchi wakadanganya mara wakasema tumeiuza kwa miaka mia sasa hivi tumewazidi kwa hoja wameondoka kwenye ile miaka mia sasa wanasema yasiyokuwepo”


“Nataka niwaambieni ndugu zangu mama ni mwaminifu, mama ni mwadilifu wala mama hawezi kufanya kitendo cha ovyo kwa familia yake” 


Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ndio kinara wetu nasi tutamuunga mkono kwa namna zote kwa maendeleo ya taifa letu sasa Wazee wangu na wananchi wenzangu kazi tuliyonayo ni moja tu kama mtamsikia mtu anasema maneno hayo mwambieni hatutaki maneno tunataka maendeleo” amesema Ulega.


Akizungumzia kufunguliwa na kuanza kutoa huduma za afya katika zahanati ya Magodani ambayo ujenzi umekamilika Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Waziri Kombo amesema zahanati hiyo inatarajia kuzinguliwa August mosi mwaka huuKombo alisema Zahanati hiyo hadi kufikia siku hiyo ya August Mosi tayari vifaa na Wahudumu wa afya na madaktari watakuwa wamefika na kuanza kutoa huduma.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI