Na mwandishi wetu, Mtwara
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na mazingira Seleman Jafo ametoa siku tatu kwa mamlaka ya bandari Tanzania kuhakikisha kuwa wanasimamia mchakato wa kufanya tathimini ya mazingira katika eneo hilo.
Agizo hilo amelitoa jana mkoani Mtwara ambapo alisema kuwa pamoja na kampuni zote zinazotumia bandari hiyo kusafirishia makaa ya mawe wakisimamiwa na NEMC wahakikishe kuwa tathimini ya mazingira inafanywa kwa usahihi.
“Jambo lile sikupendezwa nalo hata kidogo kwasababu mazingira ya hapa yalikuwa hatarishi sana ndio maana nilitoa maagizo ambayo naona kwa kiasi kikubwa yametekelezwa lakini kwanini hatumalizii usajili wa cheti cha invironmental malizieni nikisaini”alihoji Jafo
kwa upande wake Meneja wa NEMC kanda ya kusini Mhandisi Boniphace Guni alisema kuwa atasimamia agizo hilo ili liweze kutekelezeka kwa muda uliopangwa.
Nae Meneja wa Mgodi wa makaa ya mawe wa Jitegemee Boscow Mabena alisema kuwa watafata ushauri wa wataalamu ili kudhibiti uharibifu wa mazingira unaoweza kusababishwa na makaa ya mawe.
“Tuna uwezo wa kukusanya zaidi ya tani laki tano za makaa ya mawe na tumechimba mabwawa makubwa matatu kwaajili ya kuhifadhia maji taka ambayo tunayatibu na kuyarudisha kumwagilia makaa ya mawe”
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanal Ahmed Abbas alisema kuwa kufanya tathmini ya mazingira ni jambo la msingi naamini kuwa mimi na timu yangu ya mkoa tumepokea maagizo na tutafanyia kazi.
0 Comments