Hongera Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim na asante kwa heshima hii kubwa kwa nchi yetu.
Pichani ni Bw. Ahmed Salim Ahmed, mtoto wa Mheshimiwa Dkt. Salim Ahmed Salim, Waziri Mkuu Mstaafu akipokea nishani ya juu ya Taifa la Cape Verde ya Amilcar Cabral kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Cape Verde Mheshimiwa Dkt. Jose Maria Neves kwa niaba ya Mheshimiwa Salim Ahmed Salim.
Nishani hiyo ya Amilcar Cabral ambayo ni nishani ya juu ya Taifa la Cape Verde imetolewa na Serikali ya nchi hiyo ikitambua mchango wa Mheshimiwa Salim katika jitihada za ukombozi wa nchi hiyo kutoka katika ukoloni wa Ureno pamoja na ukombozi wa Mataifa mbalimbali barani Afrika.
0 Comments