Header Ads Widget

DKT. NDUMBARO AWAASA WANANCHI KUMTEGEMEA MUNGU

 



    Na Amon Mtega_  Songea

MBUNGE wa Jimbo la Songea Mjini ambaye pia ni Waziri wa Katiba na Sheria Dk ,Damas Ndumbaro amewaomba wakazi  wa Jimboni humo kushika mafundisho yanayotolewa na Viongozi wa Dini  zote ya kuwataka tumtegemea Mungu kwa kila jambo.


Wito huo ameutoa wakati akitoa salamu za rambirambi kwa katibu mwenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM kata ya Mshangano Braithon Nchimbi (Nayungi)ambaye amefiwa na mdogo wake Angerus Nchimbi kwa ajali ya pikipiki kugongwa na gari ambalo halikufahamika na kuzikwa makaburi ya mtaa wa Namanyigu yaliopo kwenye kata hiyo.


Dk ,Ndumbaro  ambaye alilazimika kukatisha ziara kwa muda mfupi akiwa ameongozana na Viongozi wa CCM ngazi ya Wilaya ya Songea Mjini kisha kuhudhuria mazishi ya marehemu Angerus Nchimbi amesema kuwa Viongozi wa dini zote wamekuwa wakituasa kwa kutufundisha kuwa muda wote tukaye tayari kwa kumtegemea Mungu maana duniani tunapita hatujui saa wala dakika.


Akizungumza kwenye mazishi hayo yaliyohudhuriwa na mamia ya wakazi wa maeneo mbalimbali ya Jimbo hilo na wajimbo la Madaba amesema kuwa kifo kinaumiza lakini hakina namna kwa kuwa tumeumbiwa lazima kila mmoja atafikiwa na umauti hivyo kikubwa ni kuzingatia mafundisho ya Viongozi wa dini.



Kwa upande wake kaka wa marehemu ambaye ni katibu mwenezi wa CCM kata ya Mshangano Braithon Nchimbi wakati akitoa neno la shukrani kwa walioenda kumfariji amesema kuwa anaishukuru ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini , ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Madaba linaongozwa na Mbunge Joseph Mhagama , Viongozi wa CCM wa ngazi zote kuanzia Wilaya hadi tawi pamoja na ndugu na jamaa kwa msaada walioweza kuutoa kwenye familia hiyo.


 Mwenezi Braithon akizungumzia ajali hiyo amesema kuwa ilitokea Julai 24 mwaka huu maeneo ya barabara ya Mkongotema Jimbo la Madaba inadaiwa waligongana na gari kubwa la mizigo ambalo halikuonekana huku marehemu Angerus Nchimbi alikuwa ni abiria kwenye pikipiki hiyo .


 Kaka wa marehemu amefafanua kuwa baada ya ajali hiyo wasamalia wema walimchukua ndugu yake ambaye ni marehemu na kumfikisha kituo cha Afya cha Madaba lakini alikuwa amefariki dunia ndipo ofisi ya Mbunge wa Madaba ilitoa gari lililobeba mwili hadi Jimbo la Songea mjini kwa mazishi.


Marehemu Angerus Nchimbi ambaye amezikwa makaburi ya Namanyigu kata ya Mshangano ameacha watoto wa wili na Mke mmoja .

   


       

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI