Header Ads Widget

DKT. MPANGO AKEMEA WANAUME WANAOPIGA WAJAWAZITO

 




Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 

MAKAMU wa Rais Dk.Philip Mpango amekemea tabia ya wanaume wanaipiga wake zao na kwamba tabia hiyo imechangia kuongezeka kwa watoto wanaoazaliwa  ambao hawajatimiza umri wa kuzaliwa (watoto njiti).


 

Dk.Mpango alisema hayo wilayani Buhigwe mkoani Kigoma kwa niaba ya serikali alipokuwa akipokea misaada mbalimbali iliyotolewa na taasisi ya Doris Mollel Foundation na Tume ya ushindi wa haki (FCC) kwa ajili ya kusaidia kukabili changamoto ya watoto njiti kwenye hospitali ya wilaya Buhigwe mkoani Kigoma.



Alisema kuwa tabia hiyo haikubaliki hata kidogo kwani pamoja na athari ya kiafya kwa wanawake wajawazito wanaopigwa lakini imesababisha msongo wa mawazo kwa wanawake hao hivyo kuzaa watoto ambao hawajatimiza umri.



Makamu wa Rais alisema kuwa kitendo cha Doris Mollel kuanzisha mpango wa kusaidia changamoto ya watoto njiti haina budi kuungwa mkono na watu wote na kuwataka wakuu wa wilaya,wakurugenzi wa halmashauri na waganga wakuu wa wilaya kutengeneza mipango ambayo itawawezesha kusaidia tatizo hilo.


Katika mpango wa kusaidia watoto njiti Makamu wa Raisi ameipongeza taasisi ya SAMAKIBA kwa mechi ya hisani iliyofanyika ambapo fedha zilzopatikana zimesaidia sehemu ya msaada huo.



Akizungumza wakati akikabidhi vifaa kwa Halmashauri ya wilaya Buhigwe, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya ushindani wa haki (FCC),Monica Moshi alisema kuwa tume hiyo imekabidhi vifaa tiba kwa ajili ya sekta ya afya kwenye vituo vya afya vilivyopo pembeni ya wilaya ya Buhigwe hususani vya kudhibiti vifo vitokanavyo na uzazi.

 


Moshi alitaja vifaa vilivyokabidhiwa kuwa ni Mashine 16 za kupima shinikizo la damu,vitanda saba vya kujifungulia wajawazito, vitanda viwili vya kupimia wagonjwa na vitanda vitatu vya kulalia wagonjwa, sanction mashine moja,magodoro 17 ya kulalia wagonjwa,mashuka 10,mashine mbili za kupima oksijeni,darubini moja na mashine 11 za kupima wingi wa damu Sambamba na hilo Mkurugenzi huyo alisema kuwa FCC imekabidhi mashine tano za kupima mapigo ya moyo mtoto akiwa tumboni.



Kwa upande wake Doris Mollel Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation alisema kuwa taasisi yake imeamua kusimamia na kuendesha program ya kusaidia watoto njiti kutokana na changamoto kubwa inayowakabili wajawazito wanaoijifungua watoto hao na kufanya ukuaji na malezi ya watoto hao kuwa na mashaka.



Katika hafla hiyo Doris Mollel amekabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 190 ikiwa ni sehemu ya kiasi cha shilingi bilioni 1.3 ambazo taasisi hiyo imetumia kwa ajili ya misaada ya mpango wa kusaidia watoto njiti.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI